LUGHA CHAFU, RUSHWA NA NIDHAMU YA KAZI VYALENGWA — QWARAY AWAONYA WATUMISHI
TMC NEWS TV
0:00 / 0:00
LUGHA CHAFU, RUSHWA NA NIDHAMU YA KAZI VYALENGWA — QWARAY AWAONYA WATUMISHI
96 просмотров · 4 мес. назад
TMC NEWS TV
42,3 тыс. подписчиков
96 просмотров · 4 мес. назад
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Regina Qwaray, ametoa wito kwa Wakuu wa Idara na watumishi wa umma kuzingatia maadili, nidhamu na weledi katika utendaji wa kazi zao.
Amesema baadhi ya changamoto zinazoikumba sekta ya utumishi wa umma ni pamoja na matumizi ya lugha zisizo na staha kazini, tuhuma za rushwa, pamoja na matumizi mabaya ya mifumo ya Serikali, hususan katika nyanja za teknolojia ya habari na mawasiliano.
Qwaray ameongeza kuwa vitendo hivyo vinachangia kudhoofisha ufanisi wa kazi na kuathiri taswira ya utumishi wa umma kwa wananchi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa watumishi kupewa mafunzo ya matumizi sahihi ya teknolojia pamoja na kuzingatia taratibu na maadili ya kazi.
Pia ametoa onyo kuwa watumishi watakaobainika kukiuka maadili na taratibu za utumishi watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.#tmcnews565 #UtumishiWaUmma #UtawalaBora #Tanzania #Dodoma #LughaChafu #Rushwa #Nidhamu #Serikali #BreakingNews #NewsUpdate