Перейти к содержимому

WANAFUNZI UKAMANDA NA UNADHIMU CSC WAKITA KAMBI YA UTAFITI NJOMBE

CLOUDS HABARI

0:00 / 0:00

WANAFUNZI UKAMANDA NA UNADHIMU CSC WAKITA KAMBI YA UTAFITI NJOMBE

89 просмотров · 1 дн. назад
CLOUDS HABARI
1,97 тыс. подписчиков
89 просмотров · 1 дн. назад
WANAFUNZI UKAMANDA NA UNADHIMU CSC WAKITA KAMBI YA UTAFITI NJOMBE Maafisa Wanafunzi 41 wanaochukua mafunzo ya Ukamanda na Unadhimu Tanzania(CSC)kutoka nchi za Rwanda,Uganda Zambia,Misri,Nigeria na Falmae za kiarabu wameweka kambi ya siku tano mkoani Njombe wakifanya utafiti wa kuhusu maendeleo ya kiuchumi na mahusiano yake kwenye usalama wa taifa huku majibu yatakayopatikana yakitakiwa kwenda kutumika katika kuimarisha usalama wa mataifa yao. Awali Mkuu wa msafara Kanali Omary Mussa Kimolo akiweka wazi sababu ya wanafunzi wa Ukamanda na unadhimu nchini(CSC)kutoka mataifa 6 tofauti wanaochukua mafunzo jijini Arusa,kuja Njombe kuendesha tafiti hizo katika miradi ya kiuchumi,amesema lengo kuwaandaa watumishi mahiri watakao kuja kufanya kazi za opresheni na kuwa na msaada mkubwa kwa mataifa yao huku meja Moses Obete kutoka Uganda akisema wanatamani kujua pia kwanini kuna tatizo la lishe wakati ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula . Kwa upande wake meja Moses Obete afisa ambae ni mwanafunzi wa ukamanda na unadhimu kutoka nchini Uganda na Janeth Ng'wanisanda wa Tanzania wamezungumzia tabia za mkoa wa Njombe na maeneo yatakayoguswa ili kuangazia maendeleo ya uchumi na usalama wa nchi . Moja ya maeneo yalifikiwa na timu hiyo ya Utafiti ni pamoja na kiwanda cha parachichi cha Season na hapa Adelina Aloyce ambae ni bibi shamba na Norasco Kilumile afisa kilimo halmashauri ya mji wa Njombe wametoa hisia zao kwa timu hiyo na kisha kueleza hatua zinazochukuliwa kuinua sekta ya kilimo. #Cloudsdigitalupdates