PAUL MAKONDA ATOA AGIZO YA KUKAMILIKA KWA VIVUKO MWANZA
CLOUDS HABARI
0:00 / 0:00
PAUL MAKONDA ATOA AGIZO YA KUKAMILIKA KWA VIVUKO MWANZA
528 просмотров · 15 ч назад
CLOUDS HABARI
1,97 тыс. подписчиков
528 просмотров · 15 ч назад
PAUL MAKONDA ATOA AGIZO YA KUKAMILIKA KWA VIVUKO MWANZA
Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe. Paul Makonda amemtaka Mkandarasi anayeshughulika na ujenzi wa vivuko vitano vilivyopo Jijini Mwanza ambavyo vimegharimu Bilioni 28.6 kuhakikisha vinakamilika ili viweze kuwasaidia wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Waziri Makonda ametoa agizo hilo akiwa Wilaya ya Ilemela jijini Mwanza katika Karakana ya Songoro Marine ambapo panapojengwa vivuko hivyo ikiwa ni ziara ya kikazi akimwakilisha Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye kukagua ujenzi wa Miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza CP Salumu Hamduni amemhakikishia Mhe Paul Makonda kuwa mkoa utasimamia kikamilifu ukamilishwaji huo.
Naye Mwenye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mwanza Michael Lushinge smart amesihi kuwa dira kuu ya taifa itawawezeaha wananchi wa Mwanza kunufaika na vivuko hivyo.
Akizungumzia suala hilo Msimamizi wa miradi kutoka Songoro Marine Isakwisa Samwel
amesema kuwa wapo katika hatua ya mwisho wa ukamilishwaji wa vivuko hivyo.
Katika Ziara hiyo ya Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Mhe Paul Makonda Ametembelea wilaya ya Nyamagana, Magu na Ilemela ambapo amekagua ujenzi wa vivuko vitano, upanuzi na uboreshaji wa bandari ya Mwanza Kaskazini, kukagua ujenzi wa tanki la maji fumagila, kuzindua shule ya awali na msingi bugumangala na kukagua kiwanda cha nondo cha steel vote vikiwa jijini Mwanza.
@hassan_omary3
#cloudsdigitalupdates