Перейти к содержимому

AGITF KUJIKITA KUTOA DHAMANA KURAHISISHA MIKOPO KWA WAKULIMA.

CLOUDS HABARI

0:00 / 0:00

AGITF KUJIKITA KUTOA DHAMANA KURAHISISHA MIKOPO KWA WAKULIMA.

9 просмотров · 10 ч назад
CLOUDS HABARI
1,97 тыс. подписчиков
9 просмотров · 10 ч назад
AGITF KUJIKITA KUTOA DHAMANA KURAHISISHA MIKOPO KWA WAKULIMA. Mfuko wa Udhamini wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) na Benki ya Azania wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya fedha kwa lengo la kuongeza upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, hususan wakulima wadogo, wanawake na vijana, ili kuwawezesha kuongeza uzalishaji, tija na kipato kupitia kilimo. Mkurugenzi Mtendaji wa AGITF, Mwanahiba Mzee, amesema ushirikiano huo ni sehemu ya mkakati wa mfuko huo kupanua wigo wa upatikanaji wa mikopo kwa kushirikiana na taasisi za fedha akisema AGITF itaendelea kutoa mikopo pale inapohitajika, huku ikijikita zaidi katika kutoa dhamana na kuwawezesha wakulima kupata mikopo yenye masharti nafuu kulingana na uwezo wao. Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza ushiriki wa taasisi za fedha katika kugharamia shughuli za kilimo, ili kufikia wakulima wengi zaidi na kuchangia malengo ya maendeleo ya kilimo nchini kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Biashara za Kilimo na Biashara Ndogo wa Benki ya Azania, Augustino Matutu, Amesema wakulima wanapaswa kuonyesha wanunuzi wa mazao yao na, inapowezekana, kuwa na mikataba ya mauzo ili kupunguza changamoto za soko na kuwawezesha kutumia mikopo kuongeza uzalishaji kwa tija. @jamesbunuma #CloudsDigitalupdate