KIJANA, SIASA NA NDOTO YA UBUNGE
THE YOUTH TALKS PODCAST
0:00 / 0:00
KIJANA, SIASA NA NDOTO YA UBUNGE
157 просмотров · 4 мес. назад
THE YOUTH TALKS PODCAST
267 подписчиков
157 просмотров · 4 мес. назад
Kijana, mwanafunzi wa chuo, lakini tayari alithubutu kuingia kwenye safari kubwa ya kisiasa ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge.
Kwenye episode hii ya The Youth Talks Podcast, tunazungumza na Mr. Huki kuhusu safari yake ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi, akiwa bado kijana na mwanafunzi. Anatueleza nini kilimsukuma kuingia kwenye siasa akiwa na umri mdogo, alijiandaaje, alipata wapi ujasiri, alikabiliana vipi na presha ya washiriki wenye uzoefu, ushawishi na mitandao mikubwa, pamoja na mafunzo aliyopata baada ya jina lake kutopita kwenye mchakato.
Hii ni episode ya hamasa, elimu na tafakari kwa vijana wanaotamani kuingia kwenye siasa, uongozi wa wanafunzi, uongozi wa jamii au nafasi kubwa za maamuzi.
Katika episode hii utajifunza:
Kwa nini vijana wanapaswa kushiriki kwenye siasa na uongozi
Changamoto za kijana kuingia kwenye nafasi kubwa kama ubunge
Umuhimu wa maandalizi, network, nidhamu na ujasiri
Namna ya kukabiliana na presha, kukataliwa na maneno ya watu
Ushauri kwa vijana wanaotamani kuanza safari ya kisiasa wakiwa wadogo
Hii siyo kampeni ya kisiasa. Ni mazungumzo ya kujifunza kuhusu uongozi, uthubutu na nafasi ya vijana kwenye maamuzi ya taifa.
Swali kwako:
Je, unaamini kijana wa chuo anaweza kuwa tayari kugombea nafasi kubwa kama ubunge? Tuambie maoni yako kwenye comment.
Usisahau ku-like, ku-comment, ku-share na ku-subscribe ili uendelee kupata maudhui ya kuelimisha, kuhamasisha na kuwawezesha vijana.
THE YOUTH TALKS PODCAST
Youth Voice. Youth Leadership. Youth Empowerment.
#TheYouthTalksPodcast #UniYouthTalks #VijanaNaSiasa #YouthLeadership #SiasaNaVijana #UongoziWaVijana #PodcastYaVijana #TanzaniaYouth #Ubunge #LeadershipJourney