Перейти к содержимому

🔴 TUNDURU: WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

RUVUMA TV

0:00 / 0:00

🔴 TUNDURU: WATU WATATU WAPOTEZA MAISHA KATIKA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

729 просмотров · 4 дня назад
RUVUMA TV
76,9 тыс. подписчиков
729 просмотров · 4 дня назад
Watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa katika mfululizo wa matukio yanayodaiwa kuchochewa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji wilayani Tunduru, Mkoa wa Ruvuma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco G. Chilya, amesema watu 25 wamekamatwa, ambapo wanane wanahusishwa na mauaji na 17 na vurugu. Kati yao, 10 ni wafugaji na 15 wakulima. Matukio hayo yalianza Septemba 17, 2026, na kuendelea hadi Septemba 21, yakihusisha mauaji, majeruhi na uharibifu wa mali, ikiwemo kuchomwa kwa baadhi ya ofisi za Serikali na kuharibiwa kwa gari la Polisi. Jeshi la Polisi linaendelea na operesheni na upelelezi kuwabaini wahusika wengine, huku likiwataka wananchi kutokujichukulia sheria mkononi na kuacha vitendo vya uporaji wa mifugo, uharibifu wa mazao na mali.