MHE.HEMED: AKERWA NA UCHAFU WA MITARO,ATOA WIKI MOJA
SHUKURU MEDIA
0:00 / 0:00
MHE.HEMED: AKERWA NA UCHAFU WA MITARO,ATOA WIKI MOJA
93 просмотра · 2 нед. назад
SHUKURU MEDIA
307 подписчиков
93 просмотра · 2 нед. назад
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amesema haridhishwi na hali ya uchafu katika baadhi ya mitaro ya kupitishia maji taka katika maeneo ya Mkoa wa Mjini Magharibi.
Mhe. Hemed ameyasema hayo wakati akikagua mitaro katika maeneo ya Mfenesi Mazizi, Mayugwani kwa Wagonga Vyuma, Gulioni na maeneo ya Ofisi ya zamani ya ZAWA pamoja na Makao Makuu ya ZECO.
Amesema hali hiyo inaweza kuhatarisha afya za wananchi, hasa wakati huu ambao Zanzibar inajiandaa kukabiliana na mvua kubwa zinazotarajiwa kuambatana na El Niño.
Makamu wa Pili wa Rais ametoa wiki moja kwa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kwa kushirikiana na taasisi nyingine, kuhakikisha mitaro ambayo maji hayapiti vizuri inafanyiwa matengenezo na kusafishwa.
Aidha, amelitaka Baraza la Manispaa Mjini kuhakikisha usafi unafanyika kwa endelevu, badala ya kusubiri kipindi cha tahadhari ya mvua.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Issa Mahfoudh Haji, amesema operesheni ya usafi tayari imeanza katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mjini na itaendelea, hasa katika maeneo hatarishi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Dkt. Said Haji Mrisho, amesema nguvu za pamoja zinahitajika kuhakikisha mitaro inafanyiwa matengenezo ili kuruhusu maji kupita bila vikwazo. #shukuru_media #zanzibar