Перейти к содержимому

WANANCHI WA KAWE KAMO MWANZA WALIA NA VIBAKA // RPC MUTAFUNGWA AHAWAHIKIKISHIA KUTOKOMEZA WIZI .

Butije Tv

0:00 / 0:00

WANANCHI WA KAWE KAMO MWANZA WALIA NA VIBAKA // RPC MUTAFUNGWA AHAWAHIKIKISHIA KUTOKOMEZA WIZI .

35 просмотров · 7 дней назад
Butije Tv
56 подписчиков
35 просмотров · 7 дней назад
​Wananchi wa Kata ya Kawekamo, Wilaya ya Ilemela, Jijini Mwanza wameliomba Jeshi la Polisi kuimarisha doria na ulinzi shirikishi katika maeneo yanayotajwa kuwa hatarishi kwa matukio ya wizi wa simu na mali nyingine za wananchi, hususan kwa wanawake. Wametoa kilio hicho katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, , baadhi yao wameeleza kuwa maeneo yenye giza, barabara na sehemu zilizotengwa na makazi yamekuwa changamoto kwa usalama, huku baadhi yao wakidai kuporwa mali zao hususan wakati wa usiku. ​Mmoja wa wananchi hao, Mwalimu, Happiness Maseke, ameeleza kuwa nyumbani kwake pamewahi kuvamiwa mchana wakati akiwa hayupo, ambapo geti na mlango vilivunjwa na mali mbalimbali, ikiwemo simu, godoro, mtungi wa gesi na vifaa vingine kuporwa. ​Kutokana na kuwepo vitendo hivyo, Happiness ameomba kuongezwa doria za mara kwa mara, wakieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuzuia uhalifu na kuwabaini watu wanaojihusisha na vitendo vya wizi. Kwa upande wake, Mkazi wa eneo hilo, Alexander Mchauru amesema; “Tunaomba ufumbuzi wa taa za barabarani. Hapa Mwanza itafikia mahali tutaona tu milingoti imesimama lakini hakuna taa. Sijui nani anahusika kwa sababu ni muda mrefu sana wahusika watusaidie.” ​Katika kikao hicho, pia wamezungumzia umuhimu wa ushirikiano kati yao na Jeshi la Polisi, ikiwemo kutoa taarifa kuhusu watu au makundi yanayodhaniwa kujihusisha na uhalifu bila kuwakatisha tamaa askari. ​"Wanamtaa tujirekebishe. Unakuta mimi nina mtoto ni mwizi, akikamatwa tunaenda kuwatolea maneno mabaya wakamataji. Tusifanye hivyo, tunawakatisha tamaa vijana wetu," amesema Wilielemia Jalajani. ​Akijibu kero hizo za wananchi, Kamanda Mutafungwa amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika kuhakikisha maeneo yote yanakuwa salama, akieleza kuwa usalama ni jukumu la pamoja. ​Kamanda Mutafungwa amewahakikishia kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya wahalifu na kuimarisha doria katika maeneo yenye changamoto za kiusalama, huku akiwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa Polisi kuhusu vitendo vya uhalifu na watu wanaojihusisha navyo. ​Amesema pia changamoto nyingine zilizowasilishwa na wananchi, ikiwemo hali ya maeneo yenye giza na miundombinu inayoweza kuhatarisha usalama, zinahitaji ushirikiano wa wadau mbalimbali wa serikali na jamii ili kupata ufumbuzi wa kudumu; hivyo amezichukua na ameahidi kuziwasilisha sehemu husika.