SMZ YATANGAZA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WENYE DIVISION ONE POINTI 3 HADI 5
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
SMZ YATANGAZA UFADHILI KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA WENYE DIVISION ONE POINTI 3 HADI 5
647 просмотров · 2 дн. назад
ASAM Online TV
22,6 тыс. подписчиков
647 просмотров · 2 дн. назад
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuanzia mwaka 2027 Serikali itatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wote wa kidato cha sita watakaopata daraja la kwanza (Division One) lenye pointi tatu hadi tano, ikiwa ni hatua ya kuongeza fursa za kuendelea na elimu ya juu.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya taifa ya kidato cha nne kwa mwaka 2024 na 2025, pamoja na kidato cha sita kwa mwaka 2026, iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu Zanzibar.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwahamasisha wanafunzi kuongeza bidii katika masomo na kuwapa nafasi ya kuendeleza uwezo wao wa kitaaluma bila kukwamishwa na ukosefu wa fedha.
Aidha, amesema mafanikio katika sekta ya elimu yanatokana na uwekezaji wa Serikali, ushirikiano wa wadau mbalimbali na juhudi za walimu pamoja na wanafunzi katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohamed Mussa, amesema kiwango cha wanafunzi wa kidato cha nne waliopata daraja sifuri (Division Zero) kimepungua kutoka asilimia 42.5 mwaka 2020 hadi asilimia 10 mwaka 2026.
Ameeleza kuwa mafanikio hayo yanahusishwa na uwekezaji katika miundombinu ya elimu, vifaa vya kisasa na uboreshaji wa maslahi ya walimu.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Khamis Abdallah Said, amesema ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne umeongezeka kutoka asilimia 82 mwaka 2024 hadi asilimia 92 mwaka 2025, huku idadi ya waliopata daraja la kwanza ikiongezeka kutoka 1,150 hadi 1,434.
#AsamOnlineTV #ElimuZanzibar #UfadhiliWaMasomo #HusseinAliMwinyi #Wanafunzi #ZanzibarNews #HabariZanzibar