Перейти к содержимому

MSAADA UNAHITAJI MADRASA, WANAFUNZI WANASOMA NJEE

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

MSAADA UNAHITAJI MADRASA, WANAFUNZI WANASOMA NJEE

179 просмотров · 1 дн. назад
ASAM Online TV
22,6 тыс. подписчиков
179 просмотров · 1 дн. назад
Walimu na wanafunzi wa Al-Madrasat Ihyau Ddiin iliyopo Mwanyanya, Mkoa wa Mjini Magharibi, wameiomba Serikali, taasisi binafsi na wananchi kusaidia upatikanaji wa eneo la ziada kwa ajili ya kujifunzia, kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi katika madrasa hiyo. Wakieleza changamoto hiyo, wamesema uhaba wa maeneo ya kujifunzia unaathiri mazingira ya masomo na kuwanyima baadhi ya wanafunzi nafasi nzuri ya kujifunza. Kwa mujibu wa walimu hao, madrasa hiyo ilianza ikiwa na wanafunzi 30, lakini kwa sasa ina zaidi ya wanafunzi 400 huku ikiwa na vyumba viwili tu vya kujifunzia. Hali hiyo imewalazimu baadhi ya wanafunzi kukaa nje wakati wa masomo kutokana na uhaba wa nafasi, jambo linaloibua hitaji la kupatikana kwa eneo la ziada ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuendeleza shughuli za madrasa hiyo. #AsamOnlineTV #AsamMediaGroup #Elimu #Madrasa #Mwanyaanya #Zanzibar #MsaadaWaElimu