Перейти к содержимому

Wema Sepetu Akiwasili Mahakama ya Kisutu Sakata la Madawa

Global TV Online

0:00 / 0:00

Wema Sepetu Akiwasili Mahakama ya Kisutu Sakata la Madawa

44 306 просмотров · 9 л. назад
Global TV Online
5,99 млн подписчиков
44 306 просмотров · 9 л. назад
Wema Sepetu, msanii wa filamu za kibongo aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2016, amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu kujibu tuhuma za kukutwa na madawa ya ku;evya aina ya bangi, nyumbani kwake. Akiwa mahakamani hapo, Wema alionekana kuwa kivutio cha wengi, watu kadhaa wakitaka kupata nafasi japo ya kumuona kwa karibu. Wema alikuwa miongoni mwa mastaa wakubwa Bongo, waliotajwa katika orodha ya awali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakituhumiwa kuhusika na biashara au matumizi ya madawa ya kulevya ambapo wote waliotajwa, walitakiwa kwenda kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi (Sentro). Baada ya kuripotisentro, Wema na wasanii wenzake walioitikia wito huo, waliwekwa mbaroni kwa siku kadhaa ambapo baadaye, wasanii wenzake waliachiwa lakini Wema aliendelea kushikiliwa. Baadaye alipelekwa kwa mkemia mkuu kupimwa kama anatumia madawa au la kabla ya kupandishwa kizimbani, akituhumiwa kukutwa na bangi nyumbani kwake. Baadaye, alichiwa kwa dhamana kwenye Mahakama ya Kisutu ambapo alitakiwa tena kuripoti Februari 22, 2017 ambapo kesi yake imetajwa tena. Katika video hii, Msanii wa Filamu za Kibongo, Wema Sepetu anaonekana akiwasili kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu ambapo kesi yake imesikilizwa tena.Kwa habaru zaidi, endelea kuitazama Global TV Online. Wema Sepetu| Apandishwa Kisutu| Madawa ya Kulevya|