Перейти к содержимому

ULEGA AWAASA WANAFUNZI LST KUTUMIA TEKNOLOJIA KWA TIJA

Katiba na Sheria Channel

0:00 / 0:00

ULEGA AWAASA WANAFUNZI LST KUTUMIA TEKNOLOJIA KWA TIJA

52 просмотра · 3 нед. назад
Katiba na Sheria Channel
317 подписчиков
52 просмотра · 3 нед. назад
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Abdallah Hamis Ulega, amewataka wanafunzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) kutumia maendeleo ya teknolojia, ikiwemo Akili Unde (AI), kwa manufaa yao binafsi, jamii na Taifa kwa ujumla. Waziri Ulega ametoa wito huo leo, Oktoba 15, 2026, wakati akizungumza na wanafunzi wa kundi la 43 katika Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa lengo la kujitambulisha na kufahamu majukumu, shughuli na mipango ya Taasisi hizo tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Waziri Ulega amewahimiza wanafunzi hao kutumia muda wao wa mafunzo kwa bidii, kujenga weledi na kuhakikisha wanapata maarifa na ujuzi utakaowawezesha kutekeleza majukumu yao ya kisheria kwa ufanisi baada ya kuhitimu.