VIJANA WATAKIWA KUTUMIA UJUZI WA KIDIJITALI KUPAMBANA NA UKOSEFU WA AJIRA
SHUKURU MEDIA
0:00 / 0:00
VIJANA WATAKIWA KUTUMIA UJUZI WA KIDIJITALI KUPAMBANA NA UKOSEFU WA AJIRA
71 просмотр · 2 недели назад
SHUKURU MEDIA
305 подписчиков
71 просмотр · 2 недели назад
Vijana wametakiwa kutumia fursa za mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kujiajiri kuanzisha biashara na kujikwamua kiuchumi katika kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini Tanzania.
Wito huo umetolewa na Dkt. Eng. Abdulrahim Haroun Ali aliyemwakilisha Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Prof. Abdi Talib Abdalla, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mradi wa majaribio unaolenga kuongeza fursa za ajira na kujiajiri kupitia teknolojia za kidijitali.
Dkt. Eng. Abdulrahim amesema ujuzi wa kidijitali unaweza kuwa nyenzo muhimu kwa vijana katika kuanzisha shughuli za kiuchumi na kutumia teknolojia kutengeneza fursa mpya za kujipatia kipato.
Kwa Upande wao vijana wajasiriamali wanaoshiriki mafunzo hayo wamesema matarajio yao ni kupata taaluma bora ya kidijitali itakayowawezesha kufanya biashara zao kwa mifumo ya kisasa na kujiongezea masoko.
Mafunzo hayo yamefunguliwa kupitia mkutano wa mtandao wa Zoom na kuandaliwa na kuendeshwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Morogoro Vyuo na taasisi mbalimbali, ikiwemo SUZA, Mbeya University of Science and Technology (MUST), Institute of Accountancy Arusha (IAA) na VETA Dodoma Campus, vimeshiriki katika ufunguzi huo.
Mafunzo hayo yanafanyika kuanzia Septemba 21 hadi 24, 2026, yakilenga kuwawezesha vijana kutumia teknolojia za kidijitali katika kujiajiri, kuanzisha biashara na kuongeza fursa za kiuchumi.
#Shukuru_media#Suza#Heet#tanzaniayouth#zanzibar