Перейти к содержимому

KAMISHENI YA ARDHI ZANZIBAR YAAGA RASMI NDEGE YA MRADI WA LARIS

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

KAMISHENI YA ARDHI ZANZIBAR YAAGA RASMI NDEGE YA MRADI WA LARIS

2 601 просмотр · 15 ч назад
ASAM Online TV
22,7 тыс. подписчиков
2 601 просмотр · 15 ч назад
Kamisheni ya Ardhi Zanzibar imeagana rasmi na ndege iliyotumika katika utekelezaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Ardhi (LARIS), mradi unaolenga kuimarisha usimamizi wa miradi mbalimbali ya ardhi visiwani Zanzibar. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi, Mhe. Rahma Kassim Ali, amesema mradi huo unalenga kupima ardhi na kutoa hati miliki ili kupunguza migogoro ya ardhi na kuchochea maendeleo nchini. Amewataka wananchi kushirikiana katika usimamizi wa ardhi ili kuepusha migogoro inayojitokeza katika jamii. Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar, Mussa Kombo Bakari, amesema taarifa za picha za anga zitasaidia kutambua maeneo, kupanga maeneo ya makaazi pamoja na maeneo yatakayotumika kwa utekelezaji wa miradi mingine. #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #LARIS #ArdhiZanzibar