Перейти к содержимому

IBADA YA JUMAPILI | AICT IGGC DODOMA | 16 AGOSTI 2026

AICT IGGC DODOMA

0:00 / 0:00

IBADA YA JUMAPILI | AICT IGGC DODOMA | 16 AGOSTI 2026

47 просмотров · 1 месяц назад
AICT IGGC DODOMA
100 подписчиков
47 просмотров · 1 месяц назад
SOMO KUU: MREJESHE ALIYEPOTEA LUKA 15:3–7 Mhubiri: Mwl. Butaga T. 16 AGOSTI, 2026 UTANGULIZI Mazungumzo ya Yesu na watoza ushuru na wenye dhambi kulizua manung’uniko kwa mafarisayo na waandishi wa sheria. Wakaanza kumlaumu Yesu kuwa anawakaribisha na kula na wenye dhambi. Kazi ya kuwarejesha wenye dhambi na waliopotea ni jukumu la kila mkristo. Umisheni wa kanisa letu ni kupeleka injili kwa watu wote. 1. Kupotea – Luka 15:3-4 Yesu anatoa mfano wa mchungaji anaemiliki kondoo mia na mmoja akapotea. Watu wengi wamepotea na wameshindwa kabisa kugundua kuwa wamepotea. Hawa wanahitaji mtu wa kuwarejesha kwa Bwana. Nani anatakiwa kujua kuwa wamepotea? Na utajuaje wamepotea? Kupotea kupo lakini muhimu ni kurudi. 2. Kumtafuta aliyepotea – Luka 15:4 Watu wamepotelea katika dhambi na tunajukumu la kuwatafuta kama huyu mchungaji aliyewaacha wale 99 na Kwenda kumtafuta yule mmoja. Unapomuona mkristo mwenzako haonekani kanisani tambua kuwa unajukumu la kumrejesha. Kazi ya kutafuta na kuleta watu kwa Yesu ni jukumu letu sote kwa kuwatembelea, kuwafundisha neno na kuwaombea. Watu wamepotelea kwenye uchawi, uzinzi, tamaa ya mali, ufisadi, uongo n.k 3. Kumbeba aliyepotea –Luka15:5 Tunapaswa kuwabeba wenye dhambi kwa kuendelea kuwaombea na kuwafundisha neno la Mungu bila kuchoka. Yesu anasema baada ya kondoo mmoja kupatikana alibebwa mabegani kwa furaha. Bahati mbaya sana leo hii baadhi ya waumini wakijua kuwa umeanguka dhambini watakubeba kwa kukutangaza kila mahali tena kwa furaha ili upotee zaidi. 4. Kuwashirikisha rafiki na jirani Luka15:6 Yesu anatukumbusha kuwa furaha ya kumrejesha au kumpata aliyepotea, inaleta furaha kwa jirani na rafiki zako. Jirani na rafiki zako wanashiriki furaha yako ya kumrejesha aliyepotea. Watu wengi wana mahusiano mabaya sana na Jirani zao kwa sababu ya mipaka,hali ya maisha,kutofautiana Imani n.k. Chunguza mahusiano yako na Jirani yako. • Weka mahusiano mema na rafiki na Jirani yako ili washiriki furaha Pamoja nawe. 5. Toba ya mwenye dhambi-Luka 15:7 Mtu mmoja anapotubu inaleta furaha kubwa mno mbinguni. Yesu anasema ni furaha kubwa mno mbinguni mtu mmoja anapotubu duniani kuliko wale 99 ambao hawana haja ya kutubu. Wapendwa tunayo kazi kubwa ya kuleta watu kwa Yesu ili tuisababishe hii furaha mbinguni kwenye haya maeneo ya umisheni kwa kanisa la AICT. Roho Mtakatifu atusaidie kuyafanya haya. Tafakari tangu umeamini watu wangapi umeweza kuwasaidia wamjue Mungu au umesababisha wasimjue Mungu? HITIMISHO: Tunajifunza yafuatayo: Ni kuwatambua waliopotea. Chukua hatua ya kumrejesha aliyepotea. Unawajibika kuwabeba waliopotea na sio kuwalaumu. Tunapaswa kuwapenda na kuwajali Jirani na rafiki zetu na kuwaambia Habari za Yesu. Unaipeleka furaha mbinguni unapomrejesha mwenye dhambi.