IBADA YA HITIMISH0 LA JUMA LA WANAWAKE | AICT IGGC DODOMA | 13 SEPTEMBA 2026
AICT IGGC DODOMA
0:00 / 0:00
IBADA YA HITIMISH0 LA JUMA LA WANAWAKE | AICT IGGC DODOMA | 13 SEPTEMBA 2026
58 просмотров · 2 недели назад
AICT IGGC DODOMA
100 подписчиков
58 просмотров · 2 недели назад
Karibu katika mafundisho maalum ya Hitimisho la Semina ya AICT Gileadi – Idara ya Wanawake, yenye kaulimbiu:
“KUMFANYA MUNGU KUWA PARTNER WA MAISHA”
Ndoa • Malezi • Uchumi
Mstari Mkuu: Ufunuo 3:11
“Naja upesi. Shika sana ulichonacho, asije mtu akaitwaa taji yako.”
Katika mafundisho haya tunajifunza kwamba kumfanya Mungu kuwa Partner wa maisha si kumfanya kuwa mshirika wa kutimiza matakwa yetu, bali ni kumruhusu Mungu awe Bwana na mwongozo wa maisha yetu, hasa katika maeneo matatu muhimu:
💍 NDOA – Kujenga ndoa katika uaminifu, heshima, mawasiliano, msamaha na msingi wa Neno la Mungu.
👨👩👧👦 MALEZI – Kutambua watoto kama amana kutoka kwa Mungu na kuwalea katika imani, nidhamu, uwajibikaji na maadili mema.
💰 UCHUMI – Kumheshimu Mungu katika kazi, kipato, matumizi, mipango, akiba, uwekezaji, utoaji na usimamizi wa rasilimali.
Mafundisho yanatufundisha kuwa agano na Mungu si maneno ya siku moja, bali ni uamuzi wa kuishi kwa uaminifu mbele zake kila siku.
🙏🏽 Je, uko tayari kumruhusu Mungu awe msingi wa ndoa yako, malezi yako na uchumi wako?
SHIKA SANA ULICHONACHO!
Ufunuo 3:11
👍🏽 Like | 💬 Comment | 🔔 Subscribe | 📲 Share
Mshirikishe mwingine ili naye apate kujifunza.
#AICTGileadi #IdaraYaWanawake #IbadaYaKiagano #PartnerWaMaisha #ShikaSanaUlichonacho #Ufunuo311 #Ndoa #Malezi #Uchumi #MafundishoYaBiblia