MKASA WA MTOTO WA MIEZI MINNE KUKATWA MKONO HOSPITALI YA LUMUMBA, UZEMBE WADAIWA KUWA CHANZO
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
MKASA WA MTOTO WA MIEZI MINNE KUKATWA MKONO HOSPITALI YA LUMUMBA, UZEMBE WADAIWA KUWA CHANZO
102 872 просмотра · 10 мес. назад
ASAM Online TV
22,5 тыс. подписчиков
102 872 просмотра · 10 мес. назад
Licha ya jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanywa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika kuimarisha miundombinu ya sekta mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, bado jitihada hizo zimekuwa zikisuasua kutokana na baadhi ya watendaji kutotekeleza majukumu yao ipasavyo.
Mtazamaji wa ASAM Online TV, huu ni mkasa uliyoikumba familia ya Bi. Safia Said Omar, mkazi wa Kijichi Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi. Mtoto wake wa miezi miwili, Said Abdallah Khamis, alipatwa na ugonjwa wa ghafla na alipopelekwa katika Hospitali ya Bububu Jeshini, aligunduliwa kuwa na tatizo la utumbo kuzongana. Baada ya uchunguzi, alipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Wilaya ya Lumumba ambako alifanyiwa upasuaji.
Hata hivyo, katika mazingira yaliyozua maswali mengi, upasuaji huo ulisababisha mkono wa mtoto huyo kukatwa. Familia yake inaeleza kwa masikitiko makubwa hatua hiyo na kutaka kufahamu sababu kamili za tukio hilo.
Uongozi wa Hospitali ya Lumumba umethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa chanzo cha tatizo ni mtoto kulaliwa na mama yake aliyekuwa akimhudumia.