Перейти к содержимому

Jicho la tatu. (Sheria & Taratibu) 2..

Rakims Spiritual

0:00 / 0:00

Jicho la tatu. (Sheria & Taratibu) 2..

6 603 просмотра · 2 г. назад
Rakims Spiritual
46,2 тыс. подписчиков
6 603 просмотра · 2 г. назад
#rakimsspiritual #playlist Sheria & Taratibu: 1:2 HAKUNA KUUNDA PICHA, HAKUNA KUDHANI PICHA, UELEWA PEKEE Basi katika sheria na taratibu ya pili ambayo ni muhimu kabisa katika jicho la tatu basi tunaona kwamba mtu mwenye kufungua jicho la tatu kuna mambo ambayo hatakiwi kuyafanya ikiwa ni pamoja na: Kutokuunda picha katika akili yake. Kutokudhania picha kwenye fikra yake. Ikiwa kwenye mazoezi yako haya unayoendelea nayo kuyafanya na ikakutokea mfano; Picha, Mwangaza au Mianga fulani hata kiumbe cha kiroho au chochote kile ambacho ni tofauti na hivyo, Kikaja kwenye maono yako. Basi usikijali kwa muda huo na uendelee na zoezi pekee lakini usizitengeneze kwa kuwa tu umesikia kwamba wenye kufanya mazoezi haya huona vitu fulani basi ukianza kukujia mwanga unaanza kuwewezseka na kujaribu kufikiri kuwa huenda hii ni kitu fulani. Basi usifanye hivyo usifikirie mwanga, au nuru au kiumbe chochote kinachotokea kwenye maono yako kuwa kina jambo au suala lolote au kuchambua kuwa wakati unafanya zoezi hilo ni nini hicho. Moja ya sababu ya kusema hivyo pia nikikumbuka kwa waliopo kwenye group ya meditation niliwaambia kuwa wajitahidi kutokuyumbishwa na picha au jambo lolote ambalo litatokea wakati mtu anafanya meditation ya kufungua jicho la tatu. Labda akajiwa na malaika katika zoezi lake hilo, hatajua kuwa ni malaika ambaye kamtengeneza yeye kwa akili yake au ni malaika ambaye ni malaika wa kweli. Shida sio kwamba mwenye kufanya hivyo kutengeneza malaika wake wa akili yake hataona picha au mwanga, Ataona vizuri tu. Shida inakuja pale kwenye ukweli wa kile ambacho malaika au roho hiyo itasema au kumuongoza. Je, ni roho kweli? Au ni akili yake mwenyewe ambayo mwisho wa siku itakuja kumpotosha na kumpoteza mbali.... Kwa hivyo ushauri wangu na katika taratibu na sheria ya Muongozo wa mtu kufungua jicho la tatu basi azingatie sheria ya Pili ambayo haimtaki atengeneze au kubuni picha ikiwa ni kwa matakwa ya akili yake. Hivyo tukubaliane kuwa hapa bado mtu hutakiwi kukariri pia sheria hii isipokuwa unatakiwa kuielewa pekee na uweze kuifanyia kazi kila uchao. Kama ilivyo kwa neno kuu la akilini wakati mtu akifanya meditation kuwa anatakiwa atulie, Basi ndivyo hivyo hivyo katika neno kuu la meditation ya kufungua jicho la tatu. Mtu anatakiwa awe na UELEWA (Nikimaanisha chochote kinachokuwa kinamtokea muda anafanya Zoezi hili basi awe ni Mwenye kuelewa kuwa ni Zoezi anafanya la macho na asilewe kama vile yeye ni sehemu ya maono hayo. Assume unachezea Virtual Reality (Chukua vitual reality kuwa picha zinazoendelea muda huo ni jicho la tatu lipo wazi. The more unazidi kuingia ndani zaidi kuaccess ndivyo unavyozidi kuona na ukianza kupiga kelele basi moja kwa moja mashine itazimwa. Hivyo ukireact kwenye jicho la tatu basi moja kwa moja maono yatakatika. Rakims Spiritual.