CCM IRINGA YAMFUTA KAZI KATIBU WAKE GOHA, SABABU YA MAADILI YATAJWA
Mwananchi Digital
0:00 / 0:00
CCM IRINGA YAMFUTA KAZI KATIBU WAKE GOHA, SABABU YA MAADILI YATAJWA
5 982 просмотра · 9 дн. назад
Mwananchi Digital
1,23 млн подписчиков
5 982 просмотра · 9 дн. назад
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Said Goha, amefutwa kazi na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, kwa tuhuma za maadili ikidaiwa kuchafua taswira ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Uamuzi huo umetolewa leo Septemba 26, 2026, na Chacha wakati akizungumza katika mkutano maalumu wa CCM Mkoa wa Iringa uliohusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa CCM na Jumuiya zake mwaka 2027, pamoja na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 ya chama hicho.
Chacha amesema Goha hatavuliwa majukumu ndani ya chama, bali atapangiwa jukumu jingine, huku CCM ikianza mchakato wa kumpata Katibu mpya wa Mkoa wa Iringa. Amesema kwa kipindi hiki, chama kitaendelea kuongozwa na Katibu mwingine hadi atakapopatikana atakayeziba nafasi hiyo.
Amesisitiza kuwa CCM haitamfumbia macho kiongozi au mwanachama ambaye mwenendo wake unaathiri taswira ya chama, akisisitiza umuhimu wa nidhamu na kulinda heshima ya CCM.