Перейти к содержимому

🔴WATU WATATU WAFARIKI, MELI YA MV CHAMBO YATEKETEA KWA MOTO ZIWA NYASA, MAMLAKA ZATOA UFAFANUZI

RUVUMA TV

0:00 / 0:00

🔴WATU WATATU WAFARIKI, MELI YA MV CHAMBO YATEKETEA KWA MOTO ZIWA NYASA, MAMLAKA ZATOA UFAFANUZI

214 просмотров · 16 часов назад
RUVUMA TV
76,9 тыс. подписчиков
214 просмотров · 16 часов назад
Watu watatu wamefariki dunia baada ya meli ya mizigo iitwayo MV Chambo, iliyosajiliwa nchini Msumbiji, kuungua moto alfajiri ya Oktoba 11, 2026, katika Ziwa Nyasa, umbali wa takribani maili 20 kutoka Bandari ya Mbamba Bay, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, meli hiyo ilikuwa na abiria 44 waliokuwa wakielekea Bandari ya Mitengula nchini Msumbiji. Marehemu wametambuliwa kuwa ni Yusto Chatanda, raia wa Tanzania, Joyce Chimalilo, raia wa Malawi, na Lilian Ela Luoga, mtoto mwenye uraia wa Msumbiji. Katika ajali hiyo, abiria 41 walinusurika na kuokolewa, kisha kupelekwa katika Hospitali ya Nangombo, Wilaya ya Nyasa, kwa ajili ya matibabu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri, huku miili ya marehemu ikihifadhiwa katika hospitali hiyo wakati taratibu za utambuzi na uchunguzi wa kitabibu zikiendelea. Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na idara nyingine zinazohusika, linaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo. Aidha, Jeshi la Polisi limewataka wananchi, wavuvi na wadau wa usafiri wa majini kuzingatia sheria na kanuni za usafirishaji wa majini, kuhakikisha vyombo vyao vinakaguliwa mara kwa mara na kuepuka kupakia abiria au mizigo inayozidi uwezo wa vyombo hivyo, ili kuzuia ajali zinazoweza kusababisha vifo na majeraha.