WAKAZI ZAIDI YA 1500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI IGANYA.
CLOUDS HABARI
0:00 / 0:00
WAKAZI ZAIDI YA 1500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI IGANYA.
2 просмотра · 1 дн. назад
CLOUDS HABARI
1,97 тыс. подписчиков
2 просмотра · 1 дн. назад
WAKAZI ZAIDI YA 1500 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI IGANYA.
Wananchi zaidi ya elfu moja mia tano wa Vijiji vya Iganya na Itaka Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wameondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama ambayo walikuwa wakiyafuata kwa umbali wa zaidi ya kilomita tatu baada ya kukamilika kwa mradi wa Iganya wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 250 uliotekelezwa na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Kwa kipindi cha muda mrefu wananchi hawa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji yaliyo safi na salama ambayo wamekuwa wakiyafuata umbali wa zaidi ya kilomita tatu na hapa baadhi yao akiwemo Vumilia Shanjiwa anaelezea ahueni wanayokenda kuipata baada ya kukamilika kwa mradi huu huku Baraka Mwamlima akiomba waunganishiwe maji majumbani.
Awali akielezea shughuli zilizofanyika mpaka sasa mkandarasi aliyetekeleza mradi huu Mhandisi Beatus Buchadi amesema mradi huu umehusisha uboreshaji wa chanzo cha maji na kisima ambacho wamehifadhia mitambo ya maji.
Aidha mradi huu wa maji Iganya umetekelezwa na shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto yaani (UNICEF)pamoja na shirika la sawa na hapa msimamizi wa mradi huu kutoka shirika la sawa Mhandisi Wilhelmina Malima akielezea ukubwa wa mradi huo huku meneja wa maji Wilayani Mbozi Mhandisi Ismail Nassor akielezea hali ya upatikani wa maji kwa sasa.
@aidamatthew07.
#CloudsDigitalUpdates.