Перейти к содержимому

JOINT SERVICE-RWANGANGA-PWM|KuZingatia kwa Bidii Zaidi,TuSije TukaPotoka.14.|UVumilivu.WaEbrania 12.

Pastor Joseph Muiruri

0:00 / 0:00

JOINT SERVICE-RWANGANGA-PWM|KuZingatia kwa Bidii Zaidi,TuSije TukaPotoka.14.|UVumilivu.WaEbrania 12.

31 просмотр · 6 мес. назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
31 просмотр · 6 мес. назад
01. WaEbrania 12:1–2. MaShahidi. Tukiwa Tumezungukiwa hivyo na MaShahidi wengi, inatupasa tutupe kila uzito na dhambi zitutegazo kwa urahisi. Mbio mbele yetu inahitaji uvumilivu. Tumtazame Yesu, Mwanzilishi na Mtimizaji wa Imani yetu. Furaha iliyowekwa mbele yake ilimhamasisha kuvumilia msalaba, akaidharau aibu. Ameketi mkono wa kuume wa Kiti cha Enzi cha Bwana Mungu. Funzo. Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi: Zaburi 51:8. Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende MaPenzi Yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi Yake: Yohana 4:34. 02. WaEbrania 12:3–11. Nidhamu. Yesu alivumilia uhasama mwingi kutoka kwa wenye dhambi dhidi yake. Hatari ipo ya kuchoka na kukata tamaa. Hatujapingana bado mpaka kumwaga damu, tukishindana na dhambi. Tunasahau himizo la Bwana Mungu linalosema nasi kama wana. Inatupasa kuthamini kuadibu kwa Bwana Mungu na kutiwa moyo anapotukemea. Bwana Mungu hufanya hivyo kwa upendo, na uvumilivu wetu hudhihirisha uhusiano wetu naye. Ni kama adhabu ya mzazi, ikikosa inanabatilisha uhalali wa kuwa mwana. Tunawaheshimu wazazi wetu kwa kutuadibu. Utii wetu wa hiari kwa Baba wa roho unapaswa kuwa zaidi. Hutupatia uzima. Kwa njia hiyo tunakuwa washiriki wa utakatifu wake. Hakuna kuadibu kunakoonekana kufurahisha kwa sasa, huumiza. Baadaye huzaa matunda ya haki yenye amani. Funzo. Hata wakati wa kuwadia Neno Lake, Ahadi ya Bwana Mungu ilimjaribu: Zaburi 105:19. Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona: Yohana 16:16. 03. WaEbrania 12:12–17. Nguvu. Lazima tutie nguvu mikono iliyolegea na magoti yaliyolemaa. Tunyoshe njia za miguu yetu, ili kile kilicho kilema kisitenguke, bali kipate kuponywa. Tufuatilie amani na watu wote na utakatifu, ambazo pasipo hivyo hakuna mtu atakayemwona Bwana Mungu. Tuangalie sana asije akapungukiwa yeyote na Neema ya Bwana Mungu. Shina la uchungu laweza kuchipuka, likasababisha taabu na kuwatia unajisi wengi. Pasiwepo nafasi ya uasherati wala matusi kwa mfano wa Esau. Kwa ajili ya tonge moja la chakula aliuza haki yake ya mzaliwakwanza hivyo akapata kukataliwa baadaye. Hakupata nafasi ya toba, ijapokuwa aliitafuta kwa bidii na machozi. Funzo. Nafsi yangu imezionea shauku nyua za Bwana Mungu, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Bwana Mungu aliye hai: Zaburi 84:2. Imetupasa kuzifanya kazi Zake Yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi: Yohana 9:4. 04. WaEbrania 12:18–24. UWepo. ✓ i. WaEbrania 12:18–21. Awali. Sisi sio wa mlima unaogusika wenye moto, weusi, giza, tufani, sauti ya baragumu na sauti ya maneno. Waliofikia huu waliomba isifanyike tena, haikuwa ya kuvumilika. Mnyama yeyote akigusa mlima alipaswa kuuawa. Hata Musa alisema, aliogopa sana na kutetemeka. ✓ ii. WaEbrania 12:22–24. Sasa. Sisi ni wa Mlima Sayuni, Mji wa Bwana Mungu aliye Hai, Yerusalemu ya Mbinguni kwa maelfu yasiyohesabika ya Malaika. Kongamano Kuu la Kanisa la MZaliwaKwanza. WaShirika wamesajiliwa Mbinguni. Tuko mbele za kwa Bwana Mungu, Hakimu wa wote na Roho za wenye Haki waliokamilishwa. Yesu Kristo yupo, MPatanishi wa Agano Jipya, na Damu ya Kunyunyizwa isemayo bora kuliko ile ya Habili. Funzo. Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi: Mwanzo 4:10. Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu: Yohana 12:32. 05. WaEbrania 12:25–29. Sauti. Hatupaswi kumkataa yeye asemaye. Waliomkataa aliyesema Duniani hawakuepuka. Ni zaidi sana ya kupoteza tukimkataa Yeye asemaye kutoka Mbinguni. Ameahidi kutikisa tena, si Dunia tu bali hata Mbingu. Hii inamaanisha kuondolewa kwa vitu vinavyotikiswa, ili kutoa nafasi kwa visivyotikiswa. Tunapokea UFalme UsioTikisika, hivyo tunahitaji Neema ituwezeshe kumtumikia Bwana Mungu kwa kumpendeza, tukiwa na staha na kicho cha Mungu. Bwana Mungu wetu ni moto ulao. Funzo. Usinitenge na uso wako, Wala Roho wako MTakatifu usiniondolee: Zaburi 51:11. Yohana 6:37 Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe: Yohana 6:37. Tafakari. Maana mtafakarini sana Yeye aliyeyastahimili mapingamizi makuu namna hii ya watendao dhambi juu ya nafsi zao, msije mkachoka, mkizimia mioyoni mwenu: WaEbrania 12:3. Wazo Kuu. Kwa hiyo inyosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza, mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe: WaEbrania 12:12–13. Sala. Basi kwa kuwa tunapokea UFalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na Neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Bwana Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho: WaEbrania 12:28.