UFUNGUZI WA TANGANYIKA INTERNATIONAL EXPO 2026
TNCC BUSINESS TV
0:00 / 0:00
UFUNGUZI WA TANGANYIKA INTERNATIONAL EXPO 2026
255 просмотров · 7 дней назад
TNCC BUSINESS TV
687 подписчиков
255 просмотров · 7 дней назад
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo, amefungua rasmi Maonesho ya Biashara ya Tanganyika International Expo 2026, yakilenga kukuza biashara, uwekezaji na masoko ya kikanda.
Maonesho hayo yamewakutanisha wafanyabiashara, wazalishaji na wawekezaji kutoka Tanzania, Uganda, Zambia, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa lengo la kuibua fursa mpya za biashara na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Naibu Waziri Londo amesisitiza umuhimu wa maonesho hayo katika kukuza biashara ya mipakani na kufungua masoko mapya kwa wafanyabiashara wa nchi hizo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TNCC Mkoa wa Kigoma, Bw. Obadia Kabuga, amesema maonesho hayo ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara kutangaza bidhaa zao, kupata masoko mapya na kujenga mahusiano ya kibiashara ndani na nje ya Tanzania.
“Maonesho haya yanaendelea kuimarisha nafasi ya Kigoma kama kiungo muhimu cha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani, huku yakifungua fursa kwa wafanyabiashara kukuza biashara na uwekezaji,” amesema Kabuga.