HISTORIA YAANDIKWA KUSINI UNGUJA KUPITIA MWENGE WA UHURU
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
HISTORIA YAANDIKWA KUSINI UNGUJA KUPITIA MWENGE WA UHURU
308 просмотров · 8 часов назад
ASAM Online TV
22,5 тыс. подписчиков
308 просмотров · 8 часов назад
Mkoa wa Kusini Unguja umeibuka Mratibu Bora wa Shughuli za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, huku Wilaya ya Kati ikishika nafasi ya kwanza katika Kanda ya Tano inayojumuisha wilaya za mikoa mitano ya Zanzibar.
Mapokezi ya ushindi huo yamefanyika katika Bandari ya Malindi, yakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Hamida Mussa Khamis, aliyeeleza furaha yake kwa mafanikio hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Baada ya mapokezi hayo, msafara ulielekea katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Tunguu, kabla ya kuendelea na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kati, Dunga.
Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Mkuu wa Wilaya ya Kati, Mhe. Rajab Ali Rajab, amewapongeza vijana kwa mchango wao katika kufanikisha ushindi huo, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano na kujituma katika utekelezaji wa shughuli za Mwenge wa Uhuru.
Ushindi huo umeiweka Mkoa wa Kusini Unguja katika nafasi ya kutambuliwa kwa uratibu wa shughuli za Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
#AsamOnlineTV #MwengeWaUhuru2026 #KusiniUnguja #WilayaYaKati #ZanzibarNews #HabariZanzibar #NewsUpdate