MVUA YA DAKIKA 10 YABOMOA NYUMBA 30, KAYA 80 ZAATHIRIKA NZOVWE JIJINI MBEYA
MbeyaYetuOnlineTV
0:00 / 0:00
MVUA YA DAKIKA 10 YABOMOA NYUMBA 30, KAYA 80 ZAATHIRIKA NZOVWE JIJINI MBEYA
22 803 просмотра · 1 дн. назад
MbeyaYetuOnlineTV
255 тыс. подписчиков
22 803 просмотра · 1 дн. назад
Nyumba zipatazo 30 zimebomoka na kaya 80 kuathirika kufuatia mafuriko yaliyotokea katika Mtaa wa Nzovwe, Kata ya Nzovwe, Jijini Mbeya, baada ya mvua kubwa kunyesha kwa takribani dakika 10 na kusababisha maji kuingia katika makazi ya wananchi.
Mafuriko hayo yanadaiwa kuchangiwa na kuzibwa kwa mtaro wa awali uliokuwa ukipitisha maji, hali iliyosababisha maji kukosa njia ya kupita na kuelekea katika makazi ya wananchi, kufuatia ujenzi wa barabara kuu ya TANZAM.
Baadhi ya wananchi walioathirika na mafuriko hayo wameeleza namna walivyokumbwa na mkasa huo, wakieleza hofu na masikitiko yao kutokana na kubomoka kwa nyumba zao na kupoteza makazi ndani ya muda mfupi.
Akizungumzia chanzo cha mafuriko hayo, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Nzovwe, Edwin Mwangonji, ameeleza jinsi kuzibwa kwa mtaro wa awali kulivyochangia maji kukosa njia ya kupita na hatimaye kuingia katika makazi ya wananchi.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nzovwe, Leo Mwakapila, ameeleza takwimu za madhara yaliyobainika baada ya kutembelea maeneo yaliyoathirika, huku Polisi Kata, ASP Charles Joseph, akieleza hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi katika kuwaokoa wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo.