1.2. TEKNOLOJIA YA KIDIGITALI KUIBADILISHA HUDUMA ZA ARDHI ZANZIBAR
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
1.2. TEKNOLOJIA YA KIDIGITALI KUIBADILISHA HUDUMA ZA ARDHI ZANZIBAR
177 просмотров · 1 дн. назад
ASAM Online TV
22,7 тыс. подписчиков
177 просмотров · 1 дн. назад
Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar, Mussa Kombo Bakari, amesema kuwajengea uwezo wafanyakazi ni hatua muhimu katika kuhakikisha utekelezaji wa mradi wa Mfumo wa Usimamizi na Usajili wa Taarifa za Ardhi Zanzibar (LARIS) unafanikiwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Ameyasema hayo wakati wa mafunzo yaliyotolewa kwa wafanyakazi wa Kamisheni hiyo katika Skuli ya Tumekuja, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea wafanyakazi uelewa mpana kuhusu mradi huo, unaokusudia kuunganisha taarifa zote za ardhi katika mfumo mmoja wa kidijitali ili kurahisisha usimamizi wa ardhi na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa LARIS Zanzibar, Barnabas Seko, amesema ushiriki wa wafanyakazi wa Kamisheni ya Ardhi ni muhimu katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio na kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Ameeleza kuwa LARIS ni kifupi cha Land Administration and Registration Information System, mfumo unaolenga kuimarisha usimamizi na usajili wa taarifa za ardhi katika maeneo yote ya Zanzibar, yakiwemo Unguja na Pemba.
Nao washiriki wa mafunzo hayo wamesema maarifa waliyoyapata yatawajengea uwezo zaidi, hususan katika kutekeleza majukumu yao ya upimaji wa ardhi.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #LARIS #ArdhiZanzibar