Перейти к содержимому

WALIMU WA SHULE ZA MSINGI, MAAFISA ELIMU NGAZI YA KATA BUNDA DC WAPATIWA MAFUNZO YA KIUNZI CHA GALA

BUNDA DC OFFICIAL

0:00 / 0:00

WALIMU WA SHULE ZA MSINGI, MAAFISA ELIMU NGAZI YA KATA BUNDA DC WAPATIWA MAFUNZO YA KIUNZI CHA GALA

136 просмотров · 6 мес. назад
BUNDA DC OFFICIAL
38 подписчиков
136 просмотров · 6 мес. назад
Walimu wa darasa la pili, baadhi ya walimu wakuu pamoja na Maafisa Elimu ngazi ya kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda wamepatiwa mafunzo maalum ya uendeshaji wa upimaji kwa kutumia kifaa cha GALA, yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo katika kufundisha na kupima stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu kwa wanafunzi wa darasa la pili kupitia Mradi wa Shule Bora. Mafunzo hayo yalifanyika kwa vitendo, ambapo washiriki walipata fursa ya kujifunza kwa kufanya majaribio ya moja kwa moja kwa baadhi ya wanafunzi ili kuona namna kiunzi cha GALA kinavyofanya kazi katika mazingira halisi ya darasani. Hatua hii imewawezesha walimu kuelewa kwa undani zaidi matumizi ya kifaa hicho na namna ya kukitumia kwa ufanisi katika upimaji wa wanafunzi. Kupitia mafunzo hayo, washiriki wamejifunza namna ya kutumia kiunzi cha GALA kinachomwezesha mwalimu kuwapima wanafunzi kwa makundi kwa ufanisi, hatua inayotarajiwa kuongeza usahihi wa tathmini pamoja na kubaini mapema changamoto za wanafunzi katika ujifunzaji. Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwezeshaji wa Kitaifa wa upimaji na utumiaji wa kifaa cha GALA, Bw. Hamis Mbinga amesema kuwa ujifunzaji unaolengwa katika upimaji huo ni stadi za msingi za KKK ambazo ni kusoma, kuandika na kuhesabu. Ameeleza kuwa matumizi ya kifaa hicho yatasaidia kuokoa gharama na rasilimali, huku matokeo yatakayopatikana yakimuwezesha mwalimu kutambua maeneo yenye uhitaji mkubwa wa kuimarishwa na hivyo kuelekeza nguvu zaidi katika ufundishaji. Halmashauri imeeleza matarajio yake kuwa washiriki wa mafunzo hayo watakuwa chachu ya mabadiliko kwa walimu wengine katika shule zao, huku matumizi ya kiunzi hicho yakitarajiwa kuleta matokeo chanya katika kuinua kiwango cha umahiri wa wanafunzi katika stadi za msingi. Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Afisa Taaluma Msingi Bi. Restituta Sasita amesema kuwa lengo kuu la halmashauri ni kuona washiriki wanatumia ujuzi walioupata kuwasaidia walimu wengine, hali itakayochangia kupunguza na hatimaye kumaliza changamoto ya wanafunzi kutokujua kusoma, kuandika na kuhesabu, sambamba na kuwajengea uwezo wa kumudu stadi hizo kwa ufanisi.