KuZingatia kwa Bidii Zaidi, TuSije TukaPotoka.| 08. AmeKeti. | WaEbrania 8.
Pastor Joseph Muiruri
0:00 / 0:00
KuZingatia kwa Bidii Zaidi, TuSije TukaPotoka.| 08. AmeKeti. | WaEbrania 8.
29 просмотров · 8 месяцев назад
Pastor Joseph Muiruri
102 подписчика
29 просмотров · 8 месяцев назад
01. WaEbrania 8:1-6. Hema.
Kiini cha Jambo ni hiki: Tunaye Kuhani Mkuu, AliyeKeti Mkono wa KuUme wa Kiti cha Enzi cha UKuu Mbinguni. Yeye ni MHudumu wa PaTakatifu na wa Hema ya Kweli, IliyoJengwa si kwa mkono wa mwanadamu bali na Bwana Mungu. Kila Kuhani Mkuu huteuliwa kutoa Sadaka na Dhabihu, hivyo ilimpasa Huyu naye Awe na kitu cha KuToa. Kama angekuwa Duniani, asingekuwa Kuhani. Wapo MaKuhani wanaotoa sadaka kulingana na Torati. Hao hutumikia MFano na Kivuli cha Mambo ya Mbinguni. Ndivyo Musa alivyoagizwa na Bwana Mungu, alipokuwa karibu kutengeneza Hema. Bwana Mungu alimwambia ahakikishe anafanya kila kitu kulingana na MFano aliyeonyeshwa Mlimani. Yesu amepata Huduma iliyo Bora zaidi. Yeye pia ni MPatanishi wa Agano Bora zaidi, lililobuniwa juu ya Ahadi zilizo Bora Zaidi.
Funzo.
MsiyaKumbuke Mambo ya Kwanza, wala MsiyaTafakari Mambo ya Zamani: Isaya 43:18.
Wala HaKuna mtu atiaye Divai Mpya katika Viriba ViKuukuu; na Kama akitia, ile Divai Mpya ItaviPasua vile Viriba, Divai yenyewe ItaMwagika, na Viriba VitaHaribika. Luka 5:37.
02. WaEbrania 8:7-12. Kasoro.
Bwana Mungu aliona kuwa Agano la Kwanza lilihitaji KuBoreshwa, kwa Sababu lilikuwa na Kasoro. Anasema:
• ✓• i. Angalia, siku zinakuja, asema Bwana Mungu, nitakapofanya Agano Jipya na Nyumba ya Israeli, na Nyumba ya Yuda: Yeremia 31:31.
• ✓• ii. Si kwa MFano wa Agano lile nililolifanya na Baba zao, katika Siku ile NilipowaShika mkono, ili KuwaToa katika Nchi ya Misri; ambalo Agano Langu hilo WaliliVunja, ingawa nalikuwa Mume kwao, asema Bwana Mungu: Yeremia 31:32.
• ✓• iii. Bali Agano hili ndilo nitakalofanya Na Nyumba ya Israeli, Baada ya Siku zile, asema Bwana Mungu; NitaTia Sheria Yangu ndani yao, na katika Mioyo yao NitaiAndika; nami NitaKuwa Bwana Mungu wao, nao WataKuwa Watu Wangu: Yeremia 31:33.
• ✓• iv. Wala HawatamFundisha kila Mtu Jirani yake, na kila mtu Ndugu yake, wakisema, Mjue Bwana Mungu; kwa maana watanijua Wote, tangu mtu aliye MDogo miongoni mwao hata aliye MKubwa miongoni mwao, asema Bwana Mungu; maana NitauSamehe Uovu wao, wala Dhambi yao SitaiKumbuka tena: Yeremia 31:34.
Funzo.
Ndipo Macho ya ViPofu YataFumbuliwa, na Masikio ya Viziwi YataZibuliwa: Isaya 35:5.
Ndipo alipojibu, akawaambia, Nendeni mkamweleze Yohana hayo MliyoyaOna na KuyaSikia; ViPofu wanapata KuOna, ViWete WanaTembea, wenye UKoma WanaTakasika, ViZiwi WanaSikia, Wafu WanaFufuliwa, Maskini WanaHubiriwa Habari Njema: Luka 7:22.
03. WaEbrania 8:13. KuToweka.
Agano Jipya linafanya la Kwanza kuwa LaAwali. Kile kinachokuwa uTupu na KuuKuu kiko karibu KuToweka.
Funzo.
Ee Bwana Mungu, UniUmbie Moyo Safi, UiFanye Upya Roho IliyoTulia ndani yangu: Zaburi 51:10.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi Njia, na Kweli, na Uzima; mtu Haji kwa Baba, ila kwa Njia ya Mimi: Yohana 14:6.
Tafakari.
Basi, katika hayo tunayosema, Neno lililo Kuu ndilo hili: Tunaye Kuhani MKuu wa Namna hii, AliyeKeti Mkono wa KuUme wa Kiti cha Enzi cha UKuu Mbinguni: WaEbrania 8:1.
Wazo Kuu.
MHudumu wa PaTakatifu, na wa ile Hema ya Kweli, ambayo Bwana Mungu AliIweka wala si mwanadamu: WaEbrania 8:2.
Sala.
Lakini sasa amepata Huduma iliyo Bora Zaidi, kwa Kadiri alivyo MJumbe wa Agano lililo Bora, LililoAmriwa juu ya Ahadi zilizo Bora: WaEbrania 8:6.