MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WATAKIWA KUWA CHACHU YA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050.
Tangajiji tv
0:00 / 0:00
MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WATAKIWA KUWA CHACHU YA UTEKELEZAJI WA DIRA 2050.
83 просмотра · 8 дн. назад
Tangajiji tv
226 подписчиков
83 просмотра · 8 дн. назад
Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe. Gilbert Kalima, amesema kuwa Idara ya Maendeleo ya Jamii ni jicho muhimu katika kuhakikisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 inatekelezwa kwa ufanisi, kutokana na nafasi ya wataalam hao katika kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo.
Mhe. Kalima ameyasema hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Kuwajengea Uwezo Maafisa Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga. Amesema Maafisa Maendeleo ya Jamii wana nafasi kubwa ya kuwafikia wananchi katika ngazi mbalimbali na kuwaelimisha kuhusu fursa, wajibu na mchango wao katika kufikia malengo yaliyowekwa na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Aidha, Mhe. Kalima amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kutumia ujuzi wanaoupata katika kikao hicho kuwa chachu ya kuhamasisha ushiriki wa wananchi na kuunganisha juhudi za jamii na mipango ya maendeleo ya Serikali. Kikao hicho kimewakutanisha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na Halmashauri ya Jiji la Tanga, kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tanga Bi. Glory Malewo amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kutumia nafasi yao ya kitaalam kuwa kiungo muhimu kati ya Serikali na wananchi katika kuhamasisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Bi. Malewo Amesema wataalam wa Maendeleo ya Jamii wana jukumu la kuwafikia wananchi, kuwaelimisha na kuwawezesha kutambua fursa zilizopo pamoja na kushiriki katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo zinazolenga kuboresha maisha yao.