Перейти к содержимому

UMASIKINI USIWE SABABU YA KUKOSA LISHE BORA

Uyui FM Radio

0:00 / 0:00

UMASIKINI USIWE SABABU YA KUKOSA LISHE BORA

109 просмотров · 6 дн. назад
Uyui FM Radio
21,7 тыс. подписчиков
109 просмотров · 6 дн. назад
Afisa Lishe wa Manispaa ya Tabora, Rehema Kapile amesema familia zinaweza kupata lishe bora hata kwa kipato kidogo kwa kutumia vyakula vinavyopatikana katika mazingira yao. Akizungumza na UFR, amesema changamoto za lishe katika Manispaa hiyo ni pamoja na udumavu kwa watoto walio chini ya miaka mitano na upungufu wa damu kwa wajawazito. Amesema wanaendelea kufanya tafiti na kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kuzingatia lishe bora na kukabiliana na utapiamlo kwa watoto. Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Tabora wamesema bado wanahitaji elimu zaidi kuhusu lishe bora. Hayo yanajiri wakati Maadhimisho ya Wiki ya Lishe Kitaifa yanafanyika kuanzia Oktoba 26 hadi 30,2026 yakiwa na Kaulimbiu isemayo "Imarisha Afya: Kula kiasili , Punguza Sukari, Chumvi na Mafuta" 📻 Sikiliza Uyui FM Radio popote ulipo duniani, bofya kiungo (link) kwenye bio yetu. #2026Fanikisha #tunasambazaunyamwezi #Fanikisha #radioyetusautiyetu