Перейти к содержимому

MADEREVA BODABODA MTWARA WALALAMIKIA UKAMATAJI , POLISI WAFAFANUA

Faruku Ngonyani

0:00 / 0:00

MADEREVA BODABODA MTWARA WALALAMIKIA UKAMATAJI , POLISI WAFAFANUA

195 просмотров · 2 нед. назад
Faruku Ngonyani
923 подписчика
195 просмотров · 2 нед. назад
Baadhi ya madereva wa bodaboda wanaofanya shughuli zao katika Manispaa ya Mtwara mkoani Mtwara, wamelalamikia Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, kwa ukamataji ambao wamedai hawaridhishwi nao. Malalamiko hayo yametolewa baada ya askari wa usalama barabarani kumkamata dereva wa bodaboda aliyetenda kosa la kubeba abiria zaidi ya mmoja, jambo lililosababisha abiria mmoja kudondoka baada ya dereva huyo kukamatwa. Aidha waeleza kuwa wamekuwa wakitozwa faini kubwa inayofikia hadi shilingi elfu 70,000 kinyume cha sheria, ambapo kanuni inataka kosa moja faini iwe shilingi elfu 10,000 Akijibu hoja hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema baadhi ya waendesha bodaboda wamekuwa hawafuati sheria za barabarani hali inayopelekea kukamatwa, huku akiwataka kutii sheria bila shuruti ili kuepuka migongano baina yao.