BINTI ALIYEPATA ONE YA 6 MTWARA HATARINI KUKOSA MASOMO YA CHUO KISA UMASIKINI "BABA NI MLEMAVU"
Faida Online TV
0:00 / 0:00
BINTI ALIYEPATA ONE YA 6 MTWARA HATARINI KUKOSA MASOMO YA CHUO KISA UMASIKINI "BABA NI MLEMAVU"
8 099 просмотров · 1 день назад
Faida Online TV
23,8 тыс. подписчиков
8 099 просмотров · 1 день назад
Ni Binti aitwae Maimuna Yusufu Lukanga (Lulanga) Mkazi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Maimuna, amehitimu masomo yake ya Kidato cha Sita na kuibuka na matokeo mazuri ya Division One ya 6 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtwara (Mtwara Girls) Na kuchaguliwa kujiunga na Chuo cha Mzumbe Campus ya Dar es salaam kwenda kusomea Sheria.
Ila Maimuna, anaziona dalili za kukatishwa kwa ndoto yake ya kuwa Mwanasheria kutokana na hali ngumu ya maisha ya Familia yake na hivyo kushindwa kumkamilishia mahitaji muhimu ya Chuo Ikiwa ni pamoja na Ada.
Baba Mzazi wa Maimuna ni mlemavu wa viungo, anayeilisha Familia yake kupitia kazi yake ya kushona Viatu, hivyo hawezi kumudu kumsomesha Binti huyo pamoja na ufaulu huo.
MAHITAJI YA MAIMUNA:
Ada ni TSH. 1300,000/= kwa mwaka.
Hostel TSH. 600,000/= kwa Mwaka
Na mahitaji Madogo Madogo
Namba ya Simu ya Baba - 0784 569 693
Jina - Abed Lukanga