Перейти к содержимому

ZHSF YATOA ONYO KWA KAMPUNI BINAFSI ZISIZOWASAJILI WAFANYAKAZI

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

ZHSF YATOA ONYO KWA KAMPUNI BINAFSI ZISIZOWASAJILI WAFANYAKAZI

305 просмотров · 16 часов назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
305 просмотров · 16 часов назад
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF), Dkt. Heri Marwa, amesema Sheria Namba 1 ya mwaka 2023 inamtaka kila Mzanzibari na mkazi wa Zanzibar kuwa mwanachama wa mfuko huo. Dkt. Marwa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa ZHSF, Michenzani Mall, Wilaya ya Mjini, Unguja. Ameeleza kuwa bado kuna kampuni nyingi za binafsi ambazo hazijawasajili wafanyakazi wao katika mfuko huo wala kuwasilisha michango yao, huku baadhi zikichangia kwa niaba ya wafanyakazi wachache tu. Hali hiyo inaibua umuhimu wa waajiri kuhakikisha wanatekeleza matakwa ya sheria kwa kusajili wafanyakazi wao na kuwasilisha michango inayohitajika, ili kuwawezesha kupata huduma za afya kwa mujibu wa utaratibu wa mfuko. #ZHSF #HudumaZaAfya #Zanzibar #SheriaYaAfya #AsamOnlineTV #ZanzibarNews