SMZ YALENGA KUWADHIBITI MADALALI FEKI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
SMZ YALENGA KUWADHIBITI MADALALI FEKI
1 330 просмотров · 1 дн. назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
1 330 просмотров · 1 дн. назад
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makaazi Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ali, amesema sekta ya milki ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi, uwekezaji, uanzishaji wa ajira na maendeleo endelevu ya miji.
Amesema hayo katika kikao kilichowakutanisha wanasheria mbalimbali kujadili masuala ya kisheria yanayohusu sekta ya umiliki wa ardhi na milki Zanzibar.
Ameeleza kuwa ongezeko la mahitaji ya ardhi, nyumba za makazi na majengo ya biashara, sambamba na upanuzi wa shughuli za utalii na miundombinu, vinaifanya sekta hiyo kuwa na nafasi muhimu katika maendeleo ya Zanzibar.
Hata hivyo, amesema sekta hiyo inahitaji kuimarishwa kupitia mifumo madhubuti ya kisheria na kitaasisi itakayohakikisha uwazi, uwajibikaji na weledi, pamoja na kulinda haki za wamiliki wa milki, wawekezaji na wananchi kwa ujumla.
Amesisitiza kuwa kutungwa kwa Sheria Maalumu ya Sekta ya Milki Zanzibar ni hatua muhimu katika kuweka mfumo ulio wazi wa kusimamia na kudhibiti miamala ya milki na huduma za kitaalamu, ikiwemo udalali wa milki na usimamizi wa majengo.
Hatua hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa sekta ya milki na kuweka mazingira bora zaidi kwa uwekezaji na maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.
#Zanzibar #SektaYaMilki #Ardhi #Uwekezaji #MaendeleoYaZanzibar #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #TanzaniaNews