SKYLONG RESORT NUNGWI KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA NA UWEKEZAJI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
SKYLONG RESORT NUNGWI KUFUNGUA FURSA ZA AJIRA NA UWEKEZAJI
912 просмотров · 2 дня назад
ASAM Online TV
22,1 тыс. подписчиков
912 просмотров · 2 дня назад
Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga, amesema uzinduzi wa mradi wa Skylong Resort unaonesha namna sekta ya utalii inavyoendelea kuvutia mitaji na kufungua fursa za ajira pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi.
Mhe. Soraga ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mradi huo unaotekelezwa Nungwi, ambao unajumuisha ujenzi wa hoteli za hadhi ya nyota tano, vila pamoja na kumbi za mikutano.
Amesema mradi huo utakapokamilika utaongeza uwezo wa Zanzibar katika kupokea watalii na mikutano ya kimataifa, huku Serikali ikiwa katika mpango wa kuandaa sheria zitakazotoa mwongozo wa wazi katika ujenzi na uendeshaji wa miradi hiyo.
Aidha, amesema sheria hizo zitaweka utaratibu wa kuwalinda wawekezaji na wanunuzi, pamoja na kuhakikisha miradi ya uwekezaji inatekelezwa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Kwa upande wao, wadau wa utalii na uwekezaji Zanzibar wamesema kuimarishwa kwa mifumo ya kisheria na usimamizi wa miradi ni muhimu katika kujenga imani ya wawekezaji na kuhakikisha ukuaji wa sekta ya utalii unakuwa endelevu.
#AsamOnlineTV #Zanzibar #SkylongResort #Nungwi #Utalii #Uwekezaji #Ajira #Hoteli #Watalii #Mikutano #SisiNiJamii