Перейти к содержимому

MAAJABU YA MJI MPYA ULIOZINDULIWA KIZIMKAZI

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

MAAJABU YA MJI MPYA ULIOZINDULIWA KIZIMKAZI

3 138 просмотров · 1 месяц назад
ASAM Online TV
22,1 тыс. подписчиков
3 138 просмотров · 1 месяц назад
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa Sekta Binafsi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa makaazi bora na miradi mingine ya uwekezaji inayochochea ukuaji wa uchumi na kufungua fursa za ajira kwa wananchi. Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo tarehe 13 Agosti 2026, alipozindua na kukagua Mradi wa Makaazi wa Amani Residency uliopo Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, ikiwa ni sehemu ya matukio ya Tamasha la Kizimkazi 2026. Rais Dkt. Mwinyi amempongeza mwekezaji wa Bopar Enterprises Ltd, Bw. Said Bopar, kwa kuwekeza katika Mradi wa Amani Residency, pamoja na Mohammedi Builders Ltd kwa kazi nzuri ya ujenzi wa mradi huo. Amesema Mradi wa Amani Residency utaongeza uwezo wa Kizimkazi kupokea wageni na kutoa huduma za makaazi ya kisasa, jambo litakalochangia kuimarisha shughuli za utalii na kuongeza mvuto katika Mkoa wa Kusini Unguja. Naye, Bw. Said Bopar, mmiliki wa Mradi wa Amani Residency, amesema utekelezaji wa mradi huo umeungwa mkono na Benki ya CRDB kupitia mkopo unaofikia asilimia 70 ya gharama za mradi. Ameeleza kuwa ushirikiano wa taasisi za fedha una nafasi muhimu katika kuwezesha uwekezaji mkubwa wa Sekta Binafsi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi. #AsamOnlineTV #Zanzibar #Kizimkazi #AmaniResidency #HusseinMwinyi #Uwekezaji #SektaBinafsi #UtaliiZanzibar #Makaazi #Uchumi #Ajira #CRDB #KizimkaziFestival2026 #ZanzibarNews #HabariZanzibar #TanzaniaNews #TikTokTanzania #InstagramTanzania #Trending #FYP #ForYou #Viral #NewsUpdate