PAJE NA JAMBIANI KUPANGWA UPYA KWA MAENDELEO YA MIJI NA UCHUMI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
PAJE NA JAMBIANI KUPANGWA UPYA KWA MAENDELEO YA MIJI NA UCHUMI
1 129 просмотров · 1 день назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
1 129 просмотров · 1 день назад
Kamisheni ya Ardhi Zanzibar imefanya kikao cha kutathmini mpango wa utekelezaji wa miji ya Paje na Jambiani, unaolenga kuimarisha matumizi bora ya ardhi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo hayo.
Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Dkt. Shein, ZURA, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akizungumza baada ya kikao hicho, Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar amesema mpango huo unalenga kuweka mpangilio mzuri wa miji ya Paje na Jambiani, kwa kuzingatia mahitaji ya miji ya kisasa na kuhakikisha maendeleo yanafanyika kwa utaratibu unaofaa.
Amesema mpango huo umezingatia huduma muhimu kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa, ili miji hiyo iendelezwe kwa namna inayokidhi mahitaji ya wananchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Hamida Mussa Khamis, amesema wataendelea kusimamia matumizi ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya mradi huo na kuwahamasisha wananchi kufuata utaratibu uliowekwa na Kamisheni ya Ardhi.
Baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho wameeleza utayari wao wa kuendelea kushirikiana na Kamisheni ya Ardhi ili kuhakikisha mpango huo unatekelezwa na matumizi sahihi ya ardhi yanaimarishwa.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #KamisheniYaArdhi #Paje #Jambiani #MipangoMiji #MatumiziBoraYaArdhi #Maendeleo #Zanzibar #HabariZanzibar #NewsUpdate #Trending