Перейти к содержимому

VIJANA WAPEWA NAFASI YA KUBUNI MIRADI YA MAZINGIRA NA AJIRA ZANZIBAR

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

VIJANA WAPEWA NAFASI YA KUBUNI MIRADI YA MAZINGIRA NA AJIRA ZANZIBAR

356 просмотров · 3 дн. назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
356 просмотров · 3 дн. назад
Baraza la Jiji la Zanzibar limepokea jumla ya maombi 42 kutoka kwa vijana wanaotaka kushiriki katika Programu ya Mabadiliko ya Tabianchi kwa kutekeleza miradi yenye manufaa kwa jamii. Akizungumza na waandishi wa habari, Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar, Kamal Abdulsatar Haji, amesema baada ya kupokea maombi hayo, Baraza linaendelea na hatua za uchambuzi ili kubaini miradi inayokidhi vigezo kwa ajili ya kupewa ruzuku na kutekelezwa. Amesema programu hiyo inalenga kuunga mkono miradi itakayosaidia kuimarisha usafi wa mazingira katika Jiji la Zanzibar, utunzaji na uhifadhi wa mazingira pamoja na kulifanya Jiji kuwa la kijani zaidi. Aidha, amesema programu hiyo inatarajiwa kutoa nafasi kwa vijana kukuza vipaji na ubunifu, huku ikichangia kuongeza fursa za ajira na ujasiriamali kupitia miradi yenye manufaa kwa jamii. #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #JijiLaZanzibar #MabadilikoYaTabianchi #Vijana #Mazingira #Ajira #Ujasiriamali #Ubunifu #Zanzibar #HabariZanzibar #NewsUpdate #Trending