Перейти к содержимому

UTALII WA ZANZIBAR WAHAMISHIWA KIDIGITALI, JamboGo.Africa

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

UTALII WA ZANZIBAR WAHAMISHIWA KIDIGITALI, JamboGo.Africa

20 просмотров · 3 часа назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
20 просмотров · 3 часа назад
Teknolojia ya kidijitali inazidi kufungua milango mipya katika sekta ya utalii Zanzibar, huku jukwaa la JamboGo.Africa likitarajiwa kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa watalii, kukuza biashara na kuongeza fursa za ajira kwa wazawa. Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Dk. Nasra Nassor Omar, amesema hayo wakati wa uzinduzi wa jukwaa hilo la kidijitali uliofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, eneo la Uwanja wa Ndege. Amesema matumizi ya teknolojia ni hatua muhimu katika kukuza uchumi na kuboresha huduma za utalii, akieleza kuwa JamboGo.Africa lina uwezo wa kuwaunganisha watalii na watoa huduma mbalimbali, wakiwemo hoteli, waendeshaji wa shughuli za utalii, waandaaji wa matukio, wasanii, wabunifu na wajasiriamali. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa JamboGo.Africa, Mohamed Hassan Mitawi, amesema jukwaa hilo limeanzishwa kutokana na uhitaji wa mfumo wa kisasa utakaowawezesha waendeshaji wa utalii wa ndani kutangaza huduma zao na kufikia masoko mapana zaidi ndani na nje ya Afrika. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wawekezaji wa Utalii Zanzibar (ZATI), Suleiman Ali Mohammed, amesema chama hicho kinaunga mkono juhudi hizo, akibainisha kuwa ZATI yenye wanachama zaidi ya 700 inaweza kushirikiana na wadau wengine kutumia jukwaa hilo kukuza utalii. Ameiomba Serikali kusimamia na kuimarisha jukwaa hilo ili liwahusishe wadau wote wa sekta ya utalii na kuunganisha nguvu katika kuitangaza Zanzibar kama kivutio cha utalii. Akizungumza kwa niaba ya Zanzibar National Chamber of Commerce (ZNCC), Biubwa Omar Khamis, amesema JamboGo.Africa ni jukwaa muhimu linalolenga kuinua biashara za wazawa wa Afrika. Jukwaa hilo linafungua fursa ya kuunganisha teknolojia, biashara na utalii, huku likilenga kuwawezesha wajasiriamali na watoa huduma wa ndani kufikia wateja wengi zaidi. #JamboGoAfrica #UtaliiZanzibar #TeknolojiaYaKidijitali #AjiraKwaVijana #ZATI #ZNCC #AsamOnlineTV #ZanzibarNews