MANISPAA YA MJINI YASIMAMISHA UJENZI MCHANGANI BAADA YA MALALAMIKO YA WANANCHI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
MANISPAA YA MJINI YASIMAMISHA UJENZI MCHANGANI BAADA YA MALALAMIKO YA WANANCHI
4 289 просмотров · 1 день назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
4 289 просмотров · 1 день назад
Wananchi wa Shehia ya Mchangani, Wilaya ya Mjini, wameeleza malalamiko yao kuhusu baadhi ya shughuli za ujenzi zinazofanyika katika maeneo yao, wakidai kuwa hazizingatii nafasi za wazi na zinaathiri utekelezaji wa shughuli nyingine za kijamii.
Malalamiko hayo yametolewa katika mkutano na viongozi wao uliofanyika Uwanja wa Mkamasini, uliolenga kujadili changamoto zinazohusiana na shughuli hizo za ujenzi na kutafuta njia za kuzitatua.
Akizungumzia suala hilo, Diwani wa Wadi ya Malindi, Khadija Saleh Ali, amesema Baraza la Manispaa ya Mjini linaendelea kufuatilia shughuli za ujenzi ili kuhakikisha zinafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Amewataka wananchi kufuata utaratibu unaofaa kwa kuwasilisha malalamiko yao kupitia mamlaka husika wanapokutana na changamoto zinazohusiana na ujenzi katika maeneo yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa ya Mjini, Hasna Atai Masoud, amesema tayari hatua za kusimamisha ujenzi unaohusika zimechukuliwa, huku wahusika wakiitwa ofisini kwa ajili ya mazungumzo na kutafuta suluhu.
Aidha, amewahimiza wananchi kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapokumbana na changamoto kama hizo badala ya kujichukulia hatua zinazoweza kusababisha taharuki.
#Mchangani #ManispaaYaMjini #Zanzibar #Maendeleo #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #HabariZanzibar