Перейти к содержимому

Banda la Kilindi lapongezwa

Kilindi Matukio

0:00 / 0:00

Banda la Kilindi lapongezwa

119 просмотров · 1 месяц назад
Kilindi Matukio
26 подписчиков
119 просмотров · 1 месяц назад
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Mhe. Lt. Col. Fredrick Komba, amewapongeza wajasiriamali wanaoshiriki katika banda la maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kwa ubunifu wao wa kuongeza thamani katika bidhaa wanazozalisha. akieleza kuwa hatua hiyo inaongeza ushindani wa bidhaa sokoni. Mhe. Komba ametoa pongezi hizo leo alipofanya ziara katika banda la Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi, akiwa Mgeni Rasmi wa siku katika Maonesho ya Kanda ya Mashariki yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, mkoani Morogoro. Katika ziara hiyo, amewahimiza wajasiriamali kuendelea kuzalisha kwa tija na kuzingatia mahitaji ya soko ili bidhaa zao ziweze kushindana katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Amesema hatua hiyo itachangia kuongeza kipato cha wazalishaji, kukuza uchumi wa taifa na kuharakisha utekelezaji wa malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kwa upande wake, Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi imeendelea kutumia maonesho hayo kuonesha bidhaa mbalimbali zenye thamani zilizobuniwa na wajasiriamali wa wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha uongezaji thamani wa mazao, kukuza biashara na kuimarisha uchumi wa wananchi.