🔥 MHE OMAR SAID SHAABAN AANZA RASMI! HILI NDILO ALILOWAAMBIA WATENDAJI BAADA YA KUKABIDHIWA WIZARA
Tifu Tv
0:00 / 0:00
🔥 MHE OMAR SAID SHAABAN AANZA RASMI! HILI NDILO ALILOWAAMBIA WATENDAJI BAADA YA KUKABIDHIWA WIZARA
3 683 просмотра · 2 дн. назад
Tifu Tv
44,8 тыс. подписчиков
3 683 просмотра · 2 дн. назад
HOTUBA YA WAZIRI WA BIASHARA NA MAENDELEO YA VIWANDA ZANZIBAR
MHE. OMAR SAID SHAABAN, WAKATI ANAZUNGUMZA NA WATENDAJI NA
VIONGOZI WA WIZARA MARA BAADA YA KUKABIDHI RASMI WIZARA TAREHE 8
OKTOBA, 2026.
Assalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakaatuh, na Habarini za Asubuhi.
Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda
Zanzibar Dkt Salum Sui Hamid
Katibu Mkuu, Dkt Habiba
Naibu Katibu Mkuu, Dkt Said
Wakurugenzi,
Wakuu wa Taasisi, na
Watendaji wote wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar:
Kwanza kabisa, namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa
kutujalia uhai na afya njema asubuhi ya leo.
Shukran kwa Rais wa Zanzibar
Shukran kwa Chama changu cha ACT Wazalendo
Shukran kwa Kaimu Waziri
Pongezi kwa Naibu Waziri na Katibu Mkuu
Shukran kwa Katibu Mkuu na Watendaji wote kwa maandalizi ya Mapokezi
Leo ni siku yetu ya kwanza kuripoti rasmi ofisini kuanza safari mpya ya utumishi
wa pamoja kwa kipindi hiki cha 2026–2030. Tumekuja kufanya kazi nanyi, bega
kwa bega, tukiwa na nia moja na maono thabiti ya kuijenga Zanzibar yetu. Ni
matumaini yangu kuwa nanyi mtakuwa na maono kama ya kwetu.
Ninataka niweke wazi mapema leo mwelekeo wa uongozi wangu: Kuanzia
sasa, Wizara hii na Taasisi zake zote hazitakuwa kikwazo wala mkandamizaji
wa sekta binafsi.
1. Wajibu Wetu: Wasemaji, Wawezeshaji, na Watetezi
Sisi
hapa wizarani ni wasemaji, wawezeshaji, na watetezi wa
wafanyabiashara, wenye viwanda, na walaji.