UNDANI AJALI YA MV CHAMBO,RPC RUVUMA,ZIMAMOTO WAFUNGUKA
Toka zamani Tv
0:00 / 0:00
UNDANI AJALI YA MV CHAMBO,RPC RUVUMA,ZIMAMOTO WAFUNGUKA
1 149 просмотров · 7 дн. назад
Toka zamani Tv
156 тыс. подписчиков
1 149 просмотров · 7 дн. назад
UNDANI AJALI YA MV CHAMBO,RPC RUVUMA,ZIMAMOTO WAFUNGUKA
Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma limethibitisha kutokea kwa ajali ya meli ya MV Chambo, iliyosajiliwa nchini Msumbiji, kuungua moto alfajiri ya Oktoba 11, 2026, na kusababisha vifo vya watu watatu huku watu 41 wakiokolewa katika ajali hiyo.
Akitoa taarifa kuhusu ajali hiyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema watu watatu wamefariki dunia baada ya meli ya mizigo iitwayo MV Chambo, iliyosajiliwa nchini Msumbiji, kuungua moto alfajiri ya Oktoba 11, 2026, katika Ziwa Nyasa, ilipokuwa ikitoka katika Bandari ya Mbamba Bay, Wilaya ya Nyasa, mkoani Ruvuma. Imeelezwa kuwa meli hiyo ilikuwa na abiria 44 waliokuwa wakielekea katika Bandari ya Mitengula nchini Msumbiji.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, amewashukuru wananchi wa wilaya hiyo walioshiriki katika zoezi la uokoaji. Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuleta boti ya uokoaji katika Ziwa Nyasa, ambayo imekuwa msaada mkubwa katika tukio hilo la leo.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Ruvuma, (SSF) Melania Nyabwinyo, amewataka wananchi wanaotumia Ziwa Nyasa kwa usafiri au shughuli za kiuchumi kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu, hasa kuhusu matumizi na uvaaji wa maboya ya kujiokolea
SUBSCRIBE HERE:www.youtube.com/c/tokazamanitv?sub_co...