BAJAJI 72 ZABANWA KWA MIZIGO KUPITA KIASI.
CLOUDS HABARI
0:00 / 0:00
BAJAJI 72 ZABANWA KWA MIZIGO KUPITA KIASI.
16 просмотров · 1 день назад
CLOUDS HABARI
1,92 тыс. подписчиков
16 просмотров · 1 день назад
BAJAJI 72 ZABANWA KWA MIZIGO KUPITA KIASI.
MWANZA: Madereva wa bajaji za mizigo wanaokiuka sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarani kwa kupakia mizigo kupita kiasi wametakiwa kuacha mara moja tabia hiyo, ambayo inahatarisha usalama wao pamoja na watumiaji wengine wa barabara.
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanya msako dhidi ya madereva wanaokiuka sheria hiyo, ambapo jumla ya madereva 72 wamebainika na kufikishwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Mwanza.
Madereva hao wamefika mbele ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa, ambapo wamekiri makosa yao na kuahidi kutorudia tena kitendo cha kupakia mizigo kupita kiasi.
Katika hatua nyingine, madereva hao wameahidi kuwa mabalozi wazuri wa usalama barabarani kwa kuwaelimisha wenzao na kutoa taarifa pindi watakapobaini madereva wanaokiuka taratibu kwa kupakia mizigo kupita kiasi.
Aidha, madereva hao wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuwapatia elimu kuhusu usalama barabarani na umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazowaongoza katika shughuli zao.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi Wilbrod Mutafungwa, amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuhakikisha sheria za nchi, hususan zinazohusu usalama barabarani, zinafuatwa.
Ametoa wito kwa madereva hao kuzingatia maelekezo waliyopewa na kuhakikisha wanazingatia sheria ili kuepuka kujihusisha na makosa yanayoweza kuzuilika na ambayo yanaweza kuhatarisha maisha yao pamoja na ya watumiaji wengine wa barabara.