HAYA HAPA MAJENGO MAPYA YA KISASA - SUZA TUNGUU
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
HAYA HAPA MAJENGO MAPYA YA KISASA - SUZA TUNGUU
761 просмотр · 13 ч назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
761 просмотр · 13 ч назад
Mkurugenzi wa Mali na Huduma wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Mhandisi Hassan Khamis Hassan, amekutana na wahandisi kutoka taasisi mbalimbali kujadili mipango ya maendeleo ya miundombinu ya chuo hicho, kwa lengo la kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu ya juu.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Jengo la Utawala la SUZA yamejikita katika mipango ya ujenzi wa nyumba ya Makamu Mkuu wa Chuo, Skuli ya Elimu pamoja na majengo mengine katika kampasi mbalimbali za chuo hicho.
Mhandisi Hassan amesema kuimarika kwa miundombinu kutasaidia kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kuimarisha matumizi ya teknolojia katika elimu ya juu na kuongeza ufanisi wa shughuli za kitaaluma.
Aidha, mipango hiyo inalenga kuvutia taasisi nyingine za chuo zilizopo katika kampasi tofauti kuhamia Kampasi ya Tunguu, hatua inayotarajiwa kurahisisha uratibu wa shughuli za chuo na kuboresha utoaji wa huduma za elimu.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuendeleza miundombinu ya SUZA na kuchangia utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya Zanzibar.
#SUZA #ElimuYaJuu #Miundombinu #ZanzibarNews #AsamOnlineTV #TanzaniaNews