Перейти к содержимому

KILIMO CHA BIASHARA NA TEKNOLOJIA KUPEWA KIPAUMBELE ZANZIBAR

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

KILIMO CHA BIASHARA NA TEKNOLOJIA KUPEWA KIPAUMBELE ZANZIBAR

307 просмотров · 12 ч назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
307 просмотров · 12 ч назад
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amesema Maonesho ya Siku ya Chakula Duniani yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuibua, kuonesha na kukuza fursa zilizopo katika sekta za kilimo na ufugaji. Amesema hayo kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Chamanangwe, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba. Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Mhe. Suleiman Masoud Makame, amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kutumia mifumo ya kisayansi kuendeleza kilimo na ufugaji wa kisasa wenye tija, unaojumuisha makundi mbalimbali na unaostahimili mabadiliko ya tabianchi. Akisoma taarifa ya kitaalamu kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Afisa Mdhamini wa Wizara, Mhandisi Idrisa Hassan Abdalla, amesema wizara inaendelea kuweka juhudi za kuwawezesha wakulima na wafugaji kuachana na kilimo cha mazoea na kuelekea katika kilimo cha biashara na endelevu. Ameeleza kuwa mwelekeo huo unalenga kuongeza tija katika uzalishaji na kuimarisha manufaa ya sekta ya kilimo na ufugaji kwa wakulima, wafugaji na taifa kwa ujumla. Maonesho hayo yanatoa fursa kwa wadau kubadilishana maarifa, kuonesha teknolojia na kujifunza mbinu bora zinazoweza kuchangia maendeleo ya kilimo na ufugaji Zanzibar. #SikuYaChakulaDuniani #Kilimo #Ufugaji #Pemba #Zanzibar #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #TanzaniaNews