WATALII KUSHIRIKI KUPANDA MITI ZANZIBAR, GPS KUTUMIKA KUFUATILIA MITI HIYO
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
WATALII KUSHIRIKI KUPANDA MITI ZANZIBAR, GPS KUTUMIKA KUFUATILIA MITI HIYO
641 просмотр · 1 дн. назад
ASAM Online TV
22,7 тыс. подписчиков
641 просмотр · 1 дн. назад
Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT), kwa kushirikiana na OTESHA Foundation, imekubaliana kutekeleza kampeni ya upandaji na utunzaji wa miti milioni moja kila mwaka katika visiwa vya Unguja na Pemba, kwa lengo la kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kukuza utalii endelevu.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mtendaji wa ZCT, Arif Abbas Manji, amesema ushirikiano huo ni sehemu ya utekelezaji wa Azimio la Utalii Endelevu la mwaka 2023, linalolenga kuhakikisha ukuaji wa sekta ya utalii unaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira.
Amesema wageni watakaotembelea Zanzibar watapata fursa ya kushiriki katika upandaji miti, huku OTESHA Foundation ikiratibu shughuli za upandaji, utunzaji na ufuatiliaji wa miti hiyo kwa kutumia teknolojia ya GPS.
Kwa upande wake, Mkuu wa Usambazaji na Ushirikiano wa OTESHA Foundation, Joseph Singano, amesema mpango huo unalenga kuwashirikisha wageni, hoteli, kampuni za usafiri na wadau wengine katika kujenga urithi wa kijani wa Zanzibar.
Uzinduzi rasmi wa mpango huo unatarajiwa kufanyika Novemba 13, 2026, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Zanzibar Green Legacy Initiative katika kulinda rasilimali za asili kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #UtaliiEndelevu #UhifadhiWaMazingira #ZanzibarGreenLegacy