BODI YA MIKOPO ZANZIBAR YATOA BILIONI 45 KUSAIDIA WANAFUNZI
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
BODI YA MIKOPO ZANZIBAR YATOA BILIONI 45 KUSAIDIA WANAFUNZI
671 просмотр · 2 дня назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
671 просмотр · 2 дня назад
Elimu Zanzibar imekuwa ikitolewa bure kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari, lakini kwa baadhi ya wanafunzi wanaofaulu kuendelea na elimu ya juu, changamoto za kifedha zimekuwa kikwazo cha kutimiza ndoto zao.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar imeendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuwawezesha kuendelea na masomo yao ya elimu ya juu.
Katika Wiki ya Huduma kwa Wateja, baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameeleza namna huduma za Bodi zilivyowasaidia kufikia malengo yao ya elimu, huku wengine wakieleza uzoefu wao wa kutumia mfumo wa ZOLAS unaowawezesha kufuatilia taarifa za mikopo pamoja na marejesho.
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA wa Bodi hiyo, Abdalla Haji Faki, amesema Wiki ya Huduma kwa Wateja imekuwa fursa kwa Bodi kuwafikia wadau wake, kusikiliza maoni na kupata ushauri wa namna ya kuboresha zaidi huduma zinazotolewa.
Bodi imesema jumla ya shilingi bilioni 45 zimetengwa kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu wanaosoma ndani na nje ya nchi.
#AsamOnlineTV #ZanzibarNews #Elimu #MikopoYaElimu #BodiYaMikopo #ZOLAS #ElimuYaJuu #Wanafunzi #Zanzibar #HabariZanzibar #NewsUpdate #Trending