MABOSI ZAWA USO KWA USO NA WAFANYAKAZI, MABADILIKO MAKUBWA YANAHITAJIKA
ASAM Online TV
0:00 / 0:00
MABOSI ZAWA USO KWA USO NA WAFANYAKAZI, MABADILIKO MAKUBWA YANAHITAJIKA
957 просмотров · 3 дня назад
ASAM Online TV
22,4 тыс. подписчиков
957 просмотров · 3 дня назад
Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) imekutana na wafanyakazi wa mamlaka hiyo kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao, hatua inayolenga kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ZAWA, Mwembe Madema, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Akizungumza baada ya kikao hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZAWA, Dkt. Maudlin Cyrus Castico, amesema mamlaka hiyo imejipanga kuimarisha huduma ya maji safi na salama kwa jamii, huku akiwataka watendaji kuwajibika na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti Msaidizi wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZAWA amesema mamlaka hiyo itachukua hatua kwa wananchi ambao hawalipi bili za maji, akieleza kuwa ulipaji wa bili ni muhimu katika kuiwezesha ZAWA kuendesha na kuendeleza miradi ya maji safi na salama.
Wafanyakazi wa ZAWA kwa upande wao wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuongeza juhudi katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa Zanzibar.
#AsamOnlineTV #ZAWA #ZanzibarNews #MajiSafI #MajiSalama #HudumaKwaJamii #Zanzibar #HabariZanzibar #NewsUpdate #Trending