Перейти к содержимому

RC KASKAZINI PEMBA AIFARIJI FAMILIA YA MWANAFUNZI RAIYAN

ASAM Online TV

0:00 / 0:00

RC KASKAZINI PEMBA AIFARIJI FAMILIA YA MWANAFUNZI RAIYAN

4 938 просмотров · 1 день назад
ASAM Online TV
22,3 тыс. подписчиков
4 938 просмотров · 1 день назад
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mhe. Mgeni Khatib Yahya, amefika Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete, kuwafariji familia ya Bi. Time Ali Omar na Hemed Amour Hemed kufuatia tukio la kupotea na kuuwawa kwa mwanafunzi Raiyan Hemed wa Skuli ya Sekondari Kizimbani Wete. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mgeni amesema Serikali inaendelea kuwa pamoja na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, huku akiitaka familia kuwa na subira na uvumilivu. Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na familia katika kipindi hicho, pamoja na kutoa faraja na ushauri kwa familia inayokabiliwa na msiba huo. Kwa upande wao, Juma Hamad Khalid na Khamis Hamad Khalid, kwa niaba ya familia, wameushukuru uongozi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kufika kuwafariji na kutoa ushauri katika kipindi hicho kigumu. Ziara hiyo imekuwa sehemu ya jitihada za viongozi kuendelea kuwa karibu na familia katika kipindi cha majonzi na kutoa pole kufuatia tukio hilo. #AsamOnlineTV #ZanzibarNews #HabariZanzibar #Pemba #Wete #Finya #Kizimbani #RaiyanHemed #NewsUpdate #Zanzibar